Tetesi: Kipa Djigui Diarra mbioni kuondoka Yanga

UNAJITEKENYA NA KUCHEKA MWENYEWE.
 
Yote heri kwa Yanga, pesa iingie tuzidi kuboresha mengineyo.
 
Na zibaki kuwa tetesi, bado sipo tayari kutokumuona Diarra pale golini.
Uwanjani hakutaendeka!

Japo utafika wakati ataondoka ila sio sasa.
Aende tu
Aliondoka Mayele na bado tumetoboa
Tatizo hawa wachezaji ukiwanyenyekea sana wanaboronga angalia Chama
 
Ni golikipa wa kisasa sana Diarra, ni ngumu sana kuwapata magolikipa wa aina yake! Golikipa ambaye anaanzisha mashambulizi vizuri, footwork yake iko vizuri sana sema tu Yanga ni kubwa kuliko mchezaji!
 
Mimi ni Diarra, Aziz, Pacome & Lomalisa

Hao wakiwepo kwenye kikosi kinachoanza kama niko uwanjani naanza kununua ice cream nakula kwa amani, ila kama hawapo naanza kunywa maji 🤣🤣🤣
 
Mimi ni Diarra, Aziz, Pacome & Lomalisa

Hao wakiwepo kwenye kikosi kinachoanza kama niko uwanjani naanza kununua ice cream nakula kwa amani, ila kama hawapo naanza kunywa maji 🤣🤣🤣
😂 wanaupiga mwingi lomalisa huwa ananikosha na ball control za uhakika.
 
😂 wanaupiga mwingi lomalisa huwa ananikosha na ball control za uhakika.
Yani mpaka nimepata goosebumps, hili wengi hawalijui!

Lomalisa akituliza mpira ni habari nyingine, unaona alivyomnyanyasa Tau hadi akamfanyia madhambi Vs Ahly? Ile siku kidogo nilie nikajikaza tu aibu watu wengi 🤣🤣🤣

Cheki mambo hayo! Acheniiii
 
Naiona Yanga ikichukua ubingwa wa ligi ikiwa bado mechi 15 mkononi
 
Hahahaaaa kaeni kwa kutulia...mdaka panzi ataondoka one day
Tatizo mashabiki wengi hatutaki mchezaji pendwa aondoke kutafuta changamoto nyingine hasa za kimaslahi tunachotaka Ni acheze milele, wakati mpira Ni biashara Kama biashara nyingine Ni lazima uuze bidhaa ili kununua bidhaa nyingine

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Lomalisa kwenye ball control ni marcelo mtupu, ukija kizembe lazima uaibike, kwenda kuwania mpira na lomalisa kunahitaji nidhamu na tahadhari sana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…