Makosa yote anayofanya Kessy ni ya kimpira. Sidhani kama kuna influence yoyote ya maslahi binafsi au kutumiwa na upande wa pili.
Kwa wachambuzi makini katika mechi ngumu na zenye pressure, Kessy bado ni liability kwa Simba na anahitaji angalau misimu 2 kufikia ubora wake halisi wa kisoka. Ana kipaji kikubwa, moyo wa upambanaji, kasi, work rate nzuri na kutokata tamaa. Lakini mapungufu makubwa aliyonayo ni kiburi, kupaniki ovyo, hajifunzi haraka na pia hafanyi maamuzi sahihi kwa wakati sahihi, mfano kupiga krosi au chenga kwa wakati sahihi.
Kama anamoyo wa kuendelea kuichezea Simba, anapaswa kupewa muda na kusaidiwa zaidi ili apevuke. Naamini Simba wakiwekeza kwake hawatajuta na taifa litamfaidi muda si mrefu. Ila kama na yeye analeta issue za kuzirazira bila kukubali makosa na kujifunza zaidi, asepe zake akatafute maisha atakako.