Kipande cha barabara cha mita 200 Tabata Kimanga chatumia miaka 10 kuwekwa lami

Kipande cha barabara cha mita 200 Tabata Kimanga chatumia miaka 10 kuwekwa lami

Update: 28/01/2020
Baada ya uzi huu tu kwenda hewani, siku mbili baadae malori mamia kwa mamia yalipishana kupeleka kokoto za lami, na leo naona kijiko kimesambaza kokoto hizo tayari kwa kushindiliwa na kumwagwa lami, ngoja tuone mwisho wake
Walianza juzi J2 kusambaza vifusi walivyomwaga wiki moja nyuma. Jana J3 na leo J4 sijapita njia hiyo kuona progress.
 
Walianza juzi J2 kusambaza vifusi walivyomwaga wiki moja nyuma. Jana J3 na leo J4 sijapita njia hiyo kuona progress.
Ngoja tuone kama lami itafanikiwa kuwekwa safari hii au ile laana ya bibi bado ipo..
 
Hadi leo mkandarasi yupo site anapambana, na bodo lami haijafanikiwa kuwekwa
 
Tangu mwaka 2009 mkandarasi yupo site na anafanya kazi usiku na mchana, anafunga barabara na kupitisha magari kwenye diversion.

Kila siku vijiko na magreda naviona vinafanya kazi pale, vifusi na kokoto vinamwagwa kila kukicha, ila kipande hicho cha mita 200 huko Tabata Kimanga hakijafanikiwa kuwekwa lami.

Na huyu mkandarasi yupo hapo site tangu 2009, na tunamuona akifanya kazi kila siku. Hata leo hii mkienda pale mtamuona yuko site na vifaa vyake, ila barabara haikamiliki.

Nasikia kuna kaburi la bibi mmoja pale lilihamishwa bila kufuata mila, ndio maana lami imegoma kuwekwa.

Kwa wajuzi wa hicho kipande cha barabara hiyo Tabata Kimanga, tunaomba maelezo, ni muujiza gani unafanyika hapo?
================================
Kuna barabara nyingine nayo inaelekea itakuja kuchukua rekodi inayofana na hii unayoiongelea wewe hapa. Sitaki kuitaja kwa jina lakini ni barabara inayoachomoka kutokea Ali Hassan, inakatiza Sinza na kuingia Mororgoro road. Barabara inajengwa kwa mwendo wa kinyonga sana. Kila ukipita iko vilevile, karibia mwaka sasa. Halafu sasa imeshaanza kusababisha foleni huku Mwai Kibaki ukiwa unaelekea Ubungo kwenye interchange
 
3 Angels message,
Wewe ndio umeongea, hapo ni siasa tu, eneo hilo ni la upinzani so hutakaa uone maendeleo mpaka mwisho wa dahari.
Aisee ni mambo ya ajabu sana nilidhani ni mimi tunndo naona hio tatizo, hicho kipande ni muda mrefu, ukweli ni siasa tu mbona wanasema?sasa sijui ccm wanapita wapi, si barabara hyohyo, tusome namba wote tu mambo mengine ni aibu sana.
 
Update:29/08/2020
Hatimae jana wameanza kuweka lami, baada ya kusota kwa miaka 10, JF kiboko
 
Tangu mwaka 2009 mkandarasi yupo site na anafanya kazi usiku na mchana, anafunga barabara na kupitisha magari kwenye diversion.

Kila siku vijiko na magreda naviona vinafanya kazi pale, vifusi na kokoto vinamwagwa kila kukicha, ila kipande hicho cha mita 200 huko Tabata Kimanga hakijafanikiwa kuwekwa lami.

Na huyu mkandarasi yupo hapo site tangu 2009, na tunamuona akifanya kazi kila siku. Hata leo hii mkienda pale mtamuona yuko site na vifaa vyake, ila barabara haikamiliki.

Nasikia kuna kaburi la bibi mmoja pale lilihamishwa bila kufuata mila, ndio maana lami imegoma kuwekwa.

Kwa wajuzi wa hicho kipande cha barabara hiyo Tabata Kimanga, tunaomba maelezo, ni muujiza gani unafanyika hapo?
================================
Update:29/08/2020
Hatimae jana wameanza kuweka lami, baada ya kusota kwa miaka 10, JF kiboko
Bila kusahau njia ya vingunguti kutoka barakuda mpaka mataa ya jet ,njia mbovu ina mashimo kweli kweli
 
Back
Top Bottom