KIPANGAMANSI

KIPANGAMANSI

Uyole CTE

Member
Joined
Apr 17, 2015
Posts
7
Reaction score
12
Hapa ndio chimbuko la Kanisa la Kiinjili la Kirutheri Tanzania (KKKT) ukanda wa kusini ambayo hapo awali ilifahamika kama synod ya konde.

Wamisionari walifika katika fukwe za ziwa Nyasa wakitokea Afrika kusini wakaambaa katika safu za mlima livingstone mpaka wakafika maeneo ya kipangamansi (Lufilyo) ambapo walipendezwa sana na eneo hili kuishi na kufungua kituo (Station) mnamo mwaka 1891, kituo hiki kiliitwa wangmanz kwa kijerumani wanyakyusa wakaita Kipangamansi

Msalabu huu ni mkubwa sana unaweza pia kuonekana ukiwa maeneo ya Itete umejengwa karibu na safu za mlima Livingstone, ulijengwa kama kumbukumbu ya jubilee ya miaka 100 ya kanisa mnamo mwaka 1991, pia katika eneo hili upo msingi wa jukwaa lililotumika wakati wa jubilee.

Yapo mambo mengi sana ya kufahamu juu ya historia hii ya Kipangamansi na ujio wa urutheri Ukanda huu wasiliana nasi kwa

Email: info@uyoleculturaltourism.com
Phone: +255783545464
P. O. Box 475 Uyole Mbeya.
Website: www.uyoleculturaltourism.com
Facebook: Uyole cultural tourism enterprise
Facebook: Uyole CTE
Instagram: @uyoleculturaltourismenterprise
Twitter: @uyolecte
 

Attachments

  • kipangamansi.jpg
    kipangamansi.jpg
    94.3 KB · Views: 63
Back
Top Bottom