Kipanya na Fina Mango wako 'Live' katika kipindi cha PowerBreakfast, Clouds FM

Kipanya na Fina Mango wako 'Live' katika kipindi cha PowerBreakfast, Clouds FM

Tresor Mandala

JF-Expert Member
Joined
Aug 20, 2010
Posts
40,905
Reaction score
86,203
Miaka 15 ya Wale jamaa wa Mjengoni, 88.5.

==========

Leo Nimewasikia hawa watangazaji wabunifu na Machachari wa Radio hii ya Clouds FM ambao waliacha kazi muda mrefu sasa. Waliitwa kwa ajili ya kuadhimisha Miaka 15 ya kituo hicho tangu kuanzishwa kwake.

Nimependa uongozi wa Clouds, pamoja na tofauti zilizowahi kuwakumba baina yao, kuamua kuwaalika hawa watu kwa kuwa walikuwa na mchango mkubwa sana enzi hizo.

Nani Hakumbuki enzi za Anko Masoud kwenye kipindi cha watoto akiwa na Kaka Bonda pamoja na Marehemu Amina Chifupa? Nani amekisahau kisauti maridhawa cha Fina Mango pale Kati?

Happy Anniversary Clouds Media - Viva forever!
 
Hongera zao maana wanasambaza upendo for real
 
Hao ndio walikuwa vichwa pale Power Breakfast. Waliondoka wakabaki wa kawaida. I am sorry to say it. Sina namna nyingine.
 
Kipindi hicho nilikuwa nachelewa kwenye mishemishe bcoz of them
 
Kabisa Clouds FM radio mmefanya jambo bora. Hao walioanzisha walikuwa bora, na nyendo zao zimeendelea kufuatwa na waliopo sasa. Congrats!:clap2::clap2::clap2:
 
nimewamiss sana kina fina na masoud wa sasa ni babra tu hao wengne hamna kitu
 
Back
Top Bottom