Unajua ukisema ufanyie kazi kila research unayosoma,unaweza ukaahirisha hata kuoa/kuolewa.Badala ya kufanya utafiti ipatikane dawa ya UKIMWI,wao wanahangaika na vipara vya watu.Shit.
Ha ha ha lakini ujue kuwa kila utafiti una lengo lake na makundi au watafiti tofauti tofauti wanafanya utafiti wa aina tofauti tofauti kulingana na elimu na utaalamu wao. Hapa lengo lilikuwa ni kuangalia uhusiano kati ya vipara na uwezekano wa mtu kupata magonjwa ya moyo (coronary heart diseases), na hii itasaidia kuweza kuwatambua kwa haraka zaidi walio katika hatari ya magonjwa ya moyo na kuwatibu mapema iwezekanavyo. Majibu zaidi ya utafiti huu yanasema kuwa adhari au hatari ya kupata magonjwa ya moyo inaongezeka zaidi kulingana na ukubwa wa kipara na pia wenye vipara vya nyuma (kisogoni) ndio wako hatarini zaidi ukiwalinganisha na wenye kipara cha mbele.
Kwa mtazamo wangu ni utafiti mzuri na ambao pia unatufaa sisi tulio katika mazingira ya nchi zetu zinazoendelea kwani magonjwa yasiyoambukiza[non-communicable diseases] (eg magonjwa ya moyo) yanaongezeka kwa kasi sana na si muda mrefu (kama hatua thabiti) zisipochukuliwa magonjwa haya yatawasumbua watu wengi sana. Magonjwa mengine ya kuambukiza [communicable diseases] nayo yana nafasi yake na pia tafiti mbali mbali zinaendelea sehemu mbali mbali duniani!
Meta-analysis of six observational studies with a
total of 36 690 participants showed that vertex
baldness is associated with an increased risk of
CHD and that the relationship depends upon the
severity of baldness, while frontal baldness is not.
▪ Thus, vertex baldness might be a marker of CHD
and is more closely associated with systemic atherosclerosis
than frontal baldness.
▪ This potential relationship should be investigated
in further studies, including well-designed prospective
studies.