Kipato cha mume na Mke ni cha familia

Kipato cha mume na Mke ni cha familia

Mparee2

JF-Expert Member
Joined
Sep 2, 2012
Posts
3,092
Reaction score
5,386
Hii dhana ya kufikiri eti Kipato cha Mwanamke ni chake peke yake ila cha Mume ni cha Familia ni dhana iliyopitwa na wakati AU niseme ni dhana potofu (ya Karne ya 15)

Ikumbukwe kuwa hiyo dhana ilikuwa na maana enzi za Yesu ambapo wanawake walikuwa kazi yao ni kuzaa na kuleo familia.

Namaanisha kuwa; kutokana na mabadiliko mbalimbali yaliyopelekea wanawake wasikae tena nyumbani badala yake wapewe Fursa sawa za kusoma, Kuajiriwat, Kujiajiri na kuzalisha; ni wajibu wao sasa kushiriki kwa asilia 100% kwenye maendeleo yote ya familia.

Tuachane na wale wanaopotosha kwa kusema kipato chao ni chao ila cha Mume ndicho cha Familia kwa kutaja mistari ya Biblia; Nawauliza tu, mbona hawamalizii kusema kuwa, Biblia imewataka wakae Nyumbani wazae na kulea familia/wasifanye kazi za kuzalisha?

Ninachotaka kusema ni kuwa, Wanawake wenye vipato wasiwanyanyase wanaume kwa vipato vyao, kwani Kazi ya kulea & maendeleo ya Familia ni kazi ya Baba na Mama kwa kadri ya vipato vyao na wala sio swala za kuamua, ni WAJIBU!

Wanavyo piga kampeni za 50%/50% waongeze na malezi ya familia ni 50%/50% ili Wanaume wawaunge mkono!

Na hili Janga la ukosefu wa ajira, ukute wanawake wameajiriwa na wanaume hawana kazi; wasipo badilika wakaendelea kungangania hiyo dhana ya kutoshiriki kwa kipato cha familia, kuna janga kubwa la ukosefu wa ndoa huko mbele.

Call a spade spade and not a BIG SPOON!
 
Unapata kifurushi kizima.
1. Akiwa hana kazi, na atulie nyumbani awe 'available' kwako mme wake na watoto muda mwingi kama sio wote.✅
2. Akiwa na kazi, basi kidogo tufaidi matunda ya hiyo kazi mambo ya kuwepo mda wote mume na watoto asamehe tu. Benefit to risk ratio☑
3. Sasa huu ujinga wa nyumbani hayupo available na bado haina msaada wowote kwa familia ni ukuku sasa huo❌🚮😒
 
Ndoa ambayo kila mmoja anahisi kabisa tokea ndani ya moyo wake kuwa ana majukumu na mwenzake na they got each others' back inajenga afya bora ya akili. Fact.

Tafiti zinaonyesha kuwa mahusiano ya karibu yenye maana hulinda wazee dhidi ya magonjwa kama kupungua kumbukumbu na alzheimers....... bila kusahau moyo.

Wanaoishi peke yao ndio wenye hatari ya kubwa zaidi ya kufa kutokana na shambulio la moyo.

Faida zaidi utazipata kwa huyu jamaa

I speak from experience my father has 65+ na Hana mke zaidi ya miaka 30 na yupo energetic ,Hana ugonjwa wowote na hii mbinu lazima niitumie as to keep my mental health safe
 
I speak from experience my father has 65+ na Hana mke zaidi ya miaka 30 na yupo energetic ,Hana ugonjwa wowote na hii mbinu lazima niitumie as to keep my mental health safe
Ni experience na hatukatai labda ni kweli. Umetoa ushahidi wa shahidi wa mdomo.

Lakini kisayansi ushahidi wa mdomo ndio wa kiwango cha mwisho kupaswa kutumiwa kufanya maamuzi. Inaitwa anecdotal report.

ILiyo bora bora kutumika ni utafiti uliodhibitiwa wenye upofu maradufu na ukafanyiwa mkasimkato😆. I mean controlled double blind crossover study/research. Ndo huo wa video.

Iliyo bora kuliko zote ni mapitio ya tafiti mbalimbali. Literature review.
 
Kipato Cha familia ni kile cha Baba/mume- mengine achana nayo utakufa mapema sana
Hiyo ilikuwa applicable miaka 80 kurudi nyuma; ina maana unakariri theory ya maisha ya baba yako ambapo wanawake kazi yao ilikuwa kuzaa na kulea familia
Mimi naongelea dhana za sasa ambapo wanawake wanapata Fursa za kusoma, Kuajiriwa, Kijiajiri nk siongelei historia....
 
Kipato Cha familia ni kile cha Baba/mume- mengine achana nayo utakufa mapema sana
Kama kipato kinatumika Cha baba na mama akae nyumbani alee watoto.
Hawezi tumia muda wa familia kwa mambo yasioihusu familia.

Familia ni taasisi na lazima iwe na mgawanyo wa majukumu.

Mama - Azae na kulea watoto na mume nyumbani (akienda kazini na kuacha jukumu hili itabidi familia yake inufaike na hicho anachoenda kufanya akiacha jukumu Lake la msingi)

Baba- Ni breadwinner na mtunza nidhamu ya familia nzima yaani watoto na mama na wote wanaoishi kwenye familia yake.

Sasa kama mama anaenda kazini na kuacha jukumu la malezi kwa watu wengine ni risk kubwa na sacrifice kubwa familia inakua imefanya inapaswa kuwe na manufaa kwa kufanya hivyo.
 
Hii dhana ya kufikiri eti Kipato cha Mwanamke ni chake peke yake ila cha Mume ni cha Familia ni dhana iliyopitwa na wakati AU niseme ni dhana potofu (ya Karne ya 15)
Ikumbukwe kuwa hiyo dhana ilikuwa na maana enzi za Yesu ambapo wanawake walikuwa kazi yao ni kuzaa na kuleo familia.

Namaanisha; kutokana na mabadiliko mbalimbali yaliyopelekea wanawake wasikae tena nyumbani badala yake wapewe Fursa sawa za kusoma, Kuajiriwa na kuzalisha; Sijui wanatokea wapi tena kudai eti kipato chao ni chao ila cha Mume ndicho cha Familia kwa sababu Biblia inasema hivyo. Mbona hawasemi kuwa Biblia imewataka wakae Nyumbani walee Watoto/wasifanye kazi za kuzalisha?

Ninachotaka kusema ni kuwa, Wanawake wenye vipato wasiwanyanyase wanaume kwa vipato vyao, kwani Kazi ya kulea & maendeleo ya Familia ni kazi ya Baba na Mama kwa kadri ya vipato vyao na wala sio swala za kuamua ni WAJIBU!

Na hili Janga la ukosefu wa ajira, ukute wanawake wameajiriwa na wanaume hawana kazi; wasipo badilika wakaendelea kungangania hiyo dhana ya kutoshiriki kwa kipato cha familia, kuna janga kubwa la ndoa huko mbele.....
Call a spade spade and not a BIG SPOON!
Kuna namna ilivyo na namna tunatamani iwe

Ilivyo ni kwamba cha KE ni chake ila cha ME ni cha wote, its natural

Ila tunatamani iwe Cha KE cha wote na cha ME cha wote tu, abadan haitakaa iwe
 
Hii dhana ya kufikiri eti Kipato cha Mwanamke ni chake peke yake ila cha Mume ni cha Familia ni dhana iliyopitwa na wakati AU niseme ni dhana potofu (ya Karne ya 15)
Ikumbukwe kuwa hiyo dhana ilikuwa na maana enzi za Yesu ambapo wanawake walikuwa kazi yao ni kuzaa na kuleo familia.

Namaanisha; kutokana na mabadiliko mbalimbali yaliyopelekea wanawake wasikae tena nyumbani badala yake wapewe Fursa sawa za kusoma, Kuajiriwa na kuzalisha; Sijui wanatokea wapi tena kudai eti kipato chao ni chao ila cha Mume ndicho cha Familia kwa sababu Biblia inasema hivyo. Mbona hawasemi kuwa Biblia imewataka wakae Nyumbani walee Watoto/wasifanye kazi za kuzalisha?

Ninachotaka kusema ni kuwa, Wanawake wenye vipato wasiwanyanyase wanaume kwa vipato vyao, kwani Kazi ya kulea & maendeleo ya Familia ni kazi ya Baba na Mama kwa kadri ya vipato vyao na wala sio swala za kuamua ni WAJIBU!

Na hili Janga la ukosefu wa ajira, ukute wanawake wameajiriwa na wanaume hawana kazi; wasipo badilika wakaendelea kungangania hiyo dhana ya kutoshiriki kwa kipato cha familia, kuna janga kubwa la ndoa huko mbele.....
Call a spade spade and not a BIG SPOON!
chunguza utagundua familia ambayo mke na mume wote wanavipato mfano watumishi mwanaume utamuona yuko kama zezeta vila hana sauti kisa mke wake analipwa kama yeye chunguza utaona mwanaume mwenye heshima na furaha nyumbani kwako niyule anae muhudumia mkewe
 
Ke wanaipush sana 50/50 mpaka mashuleni na kizazi cha wavulana kinachokuzwa huko mashuleni kinacho amini ktk 50/50 kitakuja kuwaumiza sana wanawake,sababu always mwanamke hayupo tayari kushare 50/50.
 
Mwanamke kama anafanya kazi lazima matunda yake yaonekane ndani ya familia. Kinyume na hapo ni Mhujumu uchumi wa familia na anapaswa kuchukuliwa hatua Kali za kinidhamu.

Haina faida yoyote ya yeye kufanya kazi ikiwa hachangii chochote.
 
chunguza utagundua familia ambayo mke na mume wote wanavipato mfano watumishi mwanaume utamuona yuko kama zezeta vila hana sauti kisa mke wake analipwa kama yeye chunguza utaona mwanaume mwenye heshima na furaha nyumbani kwako niyule anae muhudumia mkewe

Mke aliyeajiliwa unamhudumiaje Mkuu, Mke anayefanya kazi basi Mshahara wake atajihudumia mambo yake binafsi kama saloon nakazalika, ila mahitaji ya familia kma chakula na huduma nyingne ntazifanya mm.

Kama Mke anafanya kazi, na bado chupi ni mnunulie, basi hiyo kazi haina faida yoyote kwenye familia, ni bora akae nyumbani ni muhudumie na yeye atunze familia kama mama wa nyumbani.
 
key source ni me kukaa kwenye nafasi yake haya mengine ni maelewano tu kati yenu
 
Back
Top Bottom