Kipato chako cha mwezi mmoja kinapaswa kitoshe kulipa ada ya watoto wako ya mwaka mzima. Kama sio, standard of living yako itakuwa mbovu, unajifilisi

FRESHMAN

JF-Expert Member
Joined
Sep 29, 2011
Posts
9,137
Reaction score
34,793
Habari wadau.

Binadamu ana mahitaji mengi sana, na mojawapo ya hitaji la lazima la sasa ni elimu.

karibu Mahitaji yote ya binadamu yanahitaji Fedha kupatikana.

Kipato chako kinapaswa uweze kukigawanya vizuri. Ili kila hitaji la binadamu uweze kulipata kwa wakati.. kuepuka na magonjwa ya afya ya akili.

10 % ya kipato chako kwa mwaka ambayo kwa wastani ni sawa sawa na 10% ya kipato chako kwa kila mwezi kinapaswa kiweze ku cover hitaji la elimu la watoto wako wote kwa mwaka.

Kama mzazi unapata kipato milioni 1 kwa mwezi, laki moja kila mwezi inapaswa itumike kwenye elimu dunia ya watoto wako.

Yaani kwa mwaka watoto wako wasome kwenye shule yenye ada isiyozidi milioni 1 na laki 2 kwa mwaka.

Hii kanuni itakusaidia kuweza ku alocate 90 % ya kipato chako kwenye majukumu mengine ya lazima kwa ubora.

1. Nyumba utaishi nzuri kama umepanga kodi ya miezi sita inapaswa iweze kulipwa kwa kipato chako cha mwezi mmoja tu.

Mapato ya miezi miwili yakimudu ku cover mambo mawili makubwa yaani kodi na ada..

yanakupa nafasi ya kugawanya vizuri mapato yako ya miezi 10 iliyobaki kuweza kujipa mahitaji yote ya lazima bila kukopa kopa madeni, na wala kujitesa.

Na kuweza kufanya maendeleo mengine ya kiuchumi ya familia. Kama ujenzi wa nyumba, kufungua biashara ya familia, etc

Familia itavaa mavazi bora

Familia itatibiwa hospitali bora

Kwa ufupi Familia itakuwa na standard of living nzuri bila stress
 
Siyo kwa wanaume hawa wasiotosheka na mwanamke mmoja, hapo umesahau kupigia hesabu na hela za kuhonga michepuko, mwisho wa siku wanajikuta hawawezi kuishi bila kukopa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…