Kabla ya yote unatakiwa uwe na malengo yako, unataka kusave kwa muda gani? je ni miezi 6 au mwaka au miaka?
Fahamu sababu zinazokufanya u save pesa,je unataka ufungue biashara,au unataka ununue chombo cha usafiri?
Ukishafahamu target yako (labda target n 1 year) hapo sasa piga kazi ndani ya mwezi ukipokea pesa,kaa ndani tuliza akili..
Mkononi una 150k.. Jiulize matumizi yako makubwa n nini? najua kubwa n Malazi(kodi) na msosi.. Afya n muhimu ila kwenye mwanzo mgumu wa namna hii afya Muachie Allah....
Ukishajua matumizi yako makubwa n kodi na chakula,jiulize Unaweza kuondoa kipi kati ya hivyo viwili ili kibaki kimoja?
Jibu chakuondoa n Kodi,sasa utaishi wapi? Hapa sasa ndio ule msemo wa Maana halisi ya maisha unatokea eneo hili, Hapo Rudisha room ya watu..
Kama ulikua na vitu Uza vyotee bakiza nguo zako na begi tu kama mwana apolo,vitu utanunua huko mbeleni saivi havina maana yeyote maana hata kama una hotpot huna uwezo wakupka hata wali nusu uweke so hapa Ondoa mzigo uliokuganda.
Ukishauza kila kitu ukabaki mweupe n wewe begi lako na nguo zako ndani,sasa Rudsha chumba cha watu, Chukua siku 1 anza kuzunguka huko kwa vijana wanaopga kazi either wabeba tofali au au zege au mizigo ilmrad wawe vijana wapga kazi kweli unawaona.
mfate mmoja wao au waite wote waambie ndugu zangu mimi n mwanaume mwenzenu,nmekuja Mjini sina pa kuishi ila nmekuja kufanya kazi na nimepata kazi sehemu naomba mnifadhili pakulala tu walau mwezi huu tu,nkipata kodi nitahamia kwangu nikapange..
Amini nakwambia ktk lile kundi hatokosekana mmoja mwenye imani maana umeshawambia ukweli kuwa umekuja kutafuta maisha na unaomba pakulala tu.
Utakubaliwa nina uhakika uspokubaliwa zunguka sehemu nyngine na nyngine hadi utakapokutana na yule mtu ataekuelewa,Yupo Mkuu Yupo nina uhakika 100% ujue tu namna yakujieleza na uwe mstarabu.
Ukipata pakulala sasa kipengele ktabaki kwenye msosi, eneo hili nalo si la kucheza nalo linapoteza hela haswa,sasa hakikisha marafiki zako n kina mama ntlie na usijifanye much know kuwa mkweli ukienda kwa kna mama ntlie nunua ukoko ule mzuri utauziwa,siku moja moja ule vizuri ili usipoteze afya ule vtu vya kukupa afya TU.
ishi kwa malengo naamini kwa mwezi mzima utaweza save walau 100k kama kweli utakua na akili zile za mtafutaji wa maisha,aibu acha,ukipewa chakula maswala ya kuzuga umeshiba eti unasema Asante Acha ukipata chance ya kufukia free fukia hadi cha kesho kutwa.
Mkuu miezi yako 6 tu inakutosha kupata 600k na kuanza biashara yako,ukjikaza to 1year utakua na 1.2m Mkuu maisha n safari ndefu na ili ulijue hilo ingiza utendaji ktk hii post,maisha yako unayoyaptia leo Kesho yatakua simulizi za kuchekesha,kuliza na hata kufundisha.
Pambana Mkuu,wenzako tulianza na mishahara ya 2000 per day mapito tuliyoptia ukiyaskia utajiona wewe kumbe n lakinare unamiliki milaki kwa mwezi tena uhakika...
wakat hyo 2000 nlokua nkipewa kuna siku boss anavurugwa anakuja anagomba anasema mna kazi ya kula tu hapa kazini kwangu kazi hamfanyi mnanipa hasara tu,anachukua mauzo yote anatuacha weupe... Mkuuu maisha n safari hebu ianze yako kuna utamu wake kuanza maisha kwa style yako TRUST me utanielewa siku 1 ukivuka hiki kipindi kigumu.
YES YOU CAN.