Elections 2010 Kipengele cha 'kadhi' chapigwa 'x' ilani ya CCM!

Elections 2010 Kipengele cha 'kadhi' chapigwa 'x' ilani ya CCM!

of course wamefuata ushauri ambao niliutoa mapema na nina uhakika kwenye suala la OIC watafuta vile vile.
 
Haya ni mambo ambayo Serikali ya CCM inatubiga changa la macho. CCM ipo Bara na Visiwani (Zanzibar). Haya mambo yanapaswa kungaliwa kwa Makini sana.

Mahakama ni moja ya Mhimili wa Serikali Ukisoma katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mahakama ni suala la Muungano kama ilivyo Katiba ya Jamhuri ya Muungano yenyewe ambayo ni Sheria mama ya nchi.

Katiba inatambua kwepo kwa Mahakama Kuu ya Jamhuri ya Muungano, Mahakama Kuu ya Zanzibar na Mahakama ya Rufani ya Tanzania.

Katiba inatambua kwepo kwa Mahakama Kuu ya Jamhuri ya Muungano, Mahakama Kuu ya Zanzibar na Mahakama ya Rufani ya Tanzania.

Mamlaka ya Mahakama:

Mamlaka ya Mahakama ya Jamhuri ya Muungano: yamelezwa katika Katiba kuwa yatakuwa kama ilivyoelezwa katika Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania au katika sheria nyingine yoyote ikwemo kusikiliza kila shauri la aina yoyote ambalo halifungwi na sheria nyingine kutosikilizwa na Mahakama Kuu.

Mahakama ya Rufani ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania: ni miongoni mwa Mambo ya Muungano kwa mujibu wa Nyongeza ya Kwanza ya Katiba ya Jamnhuri ya Muungano:

Mamlaka ya Mahakama ya Rufani: kusikiliza na kutoa uamuzi juu ya kila rufaa inayoletwa mbele yake kutokana na hukumu au uamuzi wa namna nyingine yoyote wa Mahakama Kuu au Mahakama ya Hakimu kwa kuzingatia utaratibu uliowekwa na Sheria iliyotungwa kwa mujibu wa masharti ya Katiba na Bunge au na Baraza la Wawakilishi la Zanzibar.Majaji wa Mahakama ya Rufani wanatoka pande zote mbili za muungano na kwa kuwa suala la Utumishi wa Umma ni la Muungano, mashrti ya ajira zao ni ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano.

Jaji wa Mahakama ya Rufani hatashika madaraka yake ila mpaka awe ameapishwa kiapo cha uaminifu na kiapo kingine chochote kinachohusika na utendaji wa kazi kitakachowekwa kwa mujibu wa sheria iliyotungwa na Bunge (sio Baraza la Wawawkilishi).

Mahakama Kuu ya Zanzibar: Uwepo wa Mahakama ya Zanzibar ni miongoni mwa masuala ambayo yanahitaji kutolewa uamuzi na theluthi tatu ya Wabunge wa Jamhuri ya Muungano na theluthi tatu ya Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi. Jaji Mkuu wa Zanzibar ambaye anateuliwa na Rais wa SMZ anatajwa kwenye Katiba ya Zanzibar ya Mwaka 1984 kuwa ndio kiongozo wa Mahakama Kuu ya Zanzibar, tofauti na Mahakama ya Kuu (Bara) ambayo inaongozwa na Jaji Kiongozi (Principle Judge). Katiba ya Zanzibar pia inaelekeza kuwa hukumu za Mahakama Kuu ya Zanzibar zinakatiwa rufaa kwenye Mahakama ya Rufaa ya Tanzania ambayo hata hivyo inazuiliwa kusikiliza rufaa zinazohusu masuala yahusuyo tafsri ya Katiba ya Zanzibar,masuala ya Sheria za Kiislamu toka Mahakama ya Kadhi na Sheria na mambo yoyote yaliyotawa na Katiba ya Zanzibar au na sheria zilizotungwa na Baraza la Wawakilishi.

Mamlaka ya Mahakama Kuu ya Zanzibar: Kutekeleza majukumu yake kwa mujibu wa Sheria zinazotumika Zanzibar na Katiba ya Zanzibar.

Mahakama ya Kadhi: Wakati Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kama ilivyorekebishwa mwaka 2005, inaitambua Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuwa ni nchi ya Kijamaa, isiyokuwa na dini (secular state) (Ibara ya 3), mfumo wa Mahakama kwa upande wa Zanzibar unahusisha pia Mahakama ya Kadhi inayoongozwa kwa Sheria za dini ya Kiislamu (Islamic Law) na ina mamlaka ya kusikiliza mashauri ya kiislamu peeke kwa mujibu wa “Sharia Law”.

Mfumo wa Mahakama hizo ya Kadhi umekuwepo tokea enzi za ukoloni mwa Mwarabu, na uwepo wake ni suala la kisiasa na Kisheria pia. CCM kama chama tawala hawawezi kusema kuwa hawawezi kuzungumzia wala kuweka katika Ilani yao suala la Mahakama ya Kadhi wakati Zanzibar ambapo pia CCM inawanachama Mahakama hizo zipo. Kwa maana nyingine ni kuwa CCM inaweza kulificha suala hili kiani ili kutoleta hoja kwa upande wa wanachama wake kule Zanzibar ambao hata hivyo walipaswwa pia kuhoji kama chama cha Mapinduzi ni cha wa Bara na Visiwani, kwa nini Ilani yake iwe inashindwa kugusi masuala ya wanachama wengine wa upande wa pili wa Muungano??.

Mahakama ya Kadhi: Wakati Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kama ilivyorekebishwa mwaka 2005, inaitambua Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuwa ni nchi ya Kijamaa, isiyokuwa na dini (secular state) (Ibara ya 3), mfumo wa Mahakama kwa upande wa Zanzibar unahusisha pia Mahakama ya Kadhi inayoongozwa kwa Sheria za dini ya Kiislamu (Islamic Law) na ina mamlaka ya kusikiliza mashauri ya kiislamu peeke kwa mujibu wa “Sharia Law”.
Mahakama (isipokuwa Mahakama ya Rufani) sio suala la Muungano. Usichanganye madesa hapa!
 
Shida ni kwamba hizi ilani hutungwa na kakikundi kadogo ka watu. Hivyo utakuta mara nyingi si mawazo ya wanachama wala si ilani ambazo wanachama wanazihitaji.

Kwa hiyo si ajabu mtu au kikundi kidogo cha watu kikataka kuingiza mambo yao kwa jina la chama.

Na hivi ndivyo ilivyofanyika kwa ilani ya sisi M mwaka 2005. Si katika mahakama ya kadhi tu, bali hata kuhusu OIC na mambo mengine.

Vyama vingine viwe makini na hili. Wajaribu kujua ni nini hasa vipaumbele vya watu kabla ya kutunga ilani za vyama vyao.

Ndio kwa umbumbu wa watanzania kutosoma ilani hizo wengi ushangilia kwamba wana ilani swafi kumbe wakijagundua baada ya uchaguzi, utasikia malalamiko kama haya ambayo hata Kikwete kashindwa kutolea ufafanuzi mbali na kutupia chama chake lawama kuwa kilimpa tu ilani aiweke kwenye mnada lakini hakuhusika kuibuni.

Taabu inakuja zaidi pale ambapo hata kuwaadhibu watu waliofanya kosa kama hilo hakufanyiki.
 
[FONT=ArialMT, sans-serif]Chanzo cha habari hii inayofuatia ni Gazeti la Majira la Tarehe 25,June,2010[/FONT]
[FONT=ArialMT, sans-serif][/FONT]
[FONT=ArialMT, sans-serif]Chama cha Mapinduzi (CCM), kimesema suala la kuundwa kwa Mahakama ya Kadhi Tanzania limepatiwa ufumbuzi na serikali ya awamu ya nne baada ya kupokea ushauri wa Tume ya Kurekebisha Sheria uliotaka jambo hilo kuachwa kwa waumini wa dini ya Kislamu. Makamu Mwenyekiti CCM Bara, Pius Msekwa, aliwaambia waandishi wa habari mjini Dodoma jana kuwa uamuzi huo umetokana na ushauri uliotolewa na Tume ya Kurekebisha Sheria iliyokuwa ikiongozwa na Jaji Ibrahimu.[/FONT]
[FONT=ArialMT, sans-serif][/FONT]
[FONT=ArialMT, sans-serif]Msekwa aliyeongozana na Katibu Mkuu wa CCM, Yusuf Makamba, alisema ahadi ya kuanzishwa kwa Mahakama ya Kadhi ilitolewa katika Ilani ya Uchaguzi ya chama chake ya mwaka 2005 hadi 2010 katika kifungu cha 108 (B).[/FONT]
[FONT=ArialMT, sans-serif][/FONT]
[FONT=ArialMT, sans-serif]Alisema kifungu hicho kinasomeka kuwa “kulipatia ufumbuzi suala la kuanzishwa kwa Mahakama ya Kadhi Tanzania Bara”[/FONT]

“[FONT=ArialMT, sans-serif]Baadhi ya watu hawakuelewa maana ya kifungu hicho ambacho kililenga katika kulitolea ufumbuzi suala hili na si kuunda chombo hicho,” alisema. Alisema katika kulitafutia ufumbuzi jambo hilo, CCM ililikabidhi suala hilo katika Serikali ya Muungano na serikali ililifanyia kazi kwa kutumia chombo chake cha Tume ya Kurekebisha sheria.[/FONT]
[FONT=ArialMT, sans-serif][/FONT]
[FONT=ArialMT, sans-serif]Alisema Serikali ikiunda mahakama hiyo itakuwa imekwenda kinyume na Katiba ya Nchi ambayo inasema serikali haina dini.[/FONT]

“[FONT=ArialMT, sans-serif]Lakini kwa kuwa suala hili linahusu taratibu za dini ya kiislamu, Waislamu wako huru kuunda mahakama hiyo ndani ya taratibu za dini yao na Waislamu wenyewe wameshajulishwa kuhusiana na uamuzi huu,” alisema Msekwa[/FONT]

My take:
Kumbe walipoliingiza suala la Mahakama ya Kadhi kwenye Ilani yao ya Uchaguzi mwaka 2005 ilikuwa tu kuwadanganya Waislam ili wazipate kura zao?Dr Ngasongwa aliye asisi mpango mzima wa Mahakama ya Kadhi dhidi ya Jumuia za Kiislam ili tu wapate kura zao anastahili adhabu gani?

CCM wanasema Serikali imelipatia tayari ufumbuzi suala la Mahakama ya Kadhi,ni ufumbuzi gani waliwapatia wanao dai mahakama ya Kadhi ili hali haijaanzishwa?

CCM wanasema kuwa Serikali haiwezi kuisaidia dhehebu fulani kuanzisha mahakama zake;je hawakujua mapema kama mahakama ya Kadhi ni suala la kidini?Kama walijua iweje basi waliingiza kwenye Ilani yao ya Uchaguzi?

Kwa kweli JK,Msekwa,Pinda,Ngasongwa na Makamba tunataka maelezo ya kina dhidi ya jambo hili sio majibu shallow kama haya ya Mzee Msekwa!
 
Mkuu unauliza wakati jibu lipo hapo juu?..rudia kipande hiki ukisome tena na tena.....

Lakini kwa kuwa suala hili linahusu taratibu za dini ya kiislamu, Waislamu wako huru kuunda mahakama hiyo ndani ya taratibu za dini yao na Waislamu wenyewe wameshajulishwa kuhusiana na uamuzi huu,” alisema Msekwa.
 
[FONT=ArialMT, sans-serif][/FONT]My take:
Kumbe walipoliingiza suala la Mahakama ya Kadhi kwenye Ilani yao ya Uchaguzi mwaka 2005 ilikuwa tu kuwadanganya Waislam ili wazipate kura zao?Dr Ngasongwa aliye asisi mpango mzima wa Mahakama ya Kadhi dhidi ya Jumuia za Kiislam ili tu wapate kura zao anastahili adhabu gani?

CCM wanasema Serikali imelipatia tayari ufumbuzi suala la Mahakama ya Kadhi,ni ufumbuzi gani waliwapatia wanao dai mahakama ya Kadhi ili hali haijaanzishwa?

CCM wanasema kuwa Serikali haiwezi kuisaidia dhehebu fulani kuanzisha mahakama zake;je hawakujua mapema kama mahakama ya Kadhi ni suala la kidini?Kama walijua iweje basi waliingiza kwenye Ilani yao ya Uchaguzi?

Kwa kweli JK,Msekwa,Pinda,Ngasongwa na Makamba tunataka maelezo ya kina dhidi ya jambo hili sio majibu shallow kama haya ya Mzee Msekwa!

Mkuu kati ya viongozi uliowataja ni Pinda labda na JK ndio wanaoweza kuongelea swala hili vizuri tukawaelewa au waka make some sense. Msekwa na Makamba watapiga porojo tu, na si watu wa kuwaamini hata kidogo and do not take their words seriously.

You can not say serikali haiwezi kuanzisha mahakama ya Kadhi at the same time unasema waislamu wanaweza kuazisha mahakama hiyohiyo, ndani ya nchi moja. It is stupid indeed and a bad precedence kwa nchi kama Tanzania kuanza kuingiza Sharia law taratibu.

Huwezi kuwaweka watanzania kwenye two sets of laws, yaani seti moja kwa ajili ya wasio waislamu (regardless of matters the sai court will deal with) na nyingine ni kwa ajili ya waislamu, hii ni hatua ya kwanza kuwagawa watanzania, we are one people and we are best when we are one. What will they say if the likes of Joseph Kony comes into Tanzanian politics, tutamlaumu nani? or will there be another stupid answer kuwa wakristo wanaweza kuanzisha mahakama yao? Ujanja wa kutaka kuwahonga waislamu tunapoelekea kwenye uchaguzi kwa kitu cha hatari kwa nchi haufai, those who push this agenda within the party and those who entertain it should be ashamed.

Kauli kama hiyo si ya kutegemea kusikia kutoka kwa mtu mwenye nafasi kama Msekwa ndani ya Chama, kusema kuwa serikali haina dini ni mawazo finyu kwa kuwa kila mtu anafahamu hilo, na hatuna haja ya kuanza kuwaambia watu, Nyerere alituambia hilo miaka ya 60 it can not be a story in 2010, hata watoto wa shule ya msingi wanajua hilo.
 
Bongoland,
Mkuu samahani kidogo hapa sijakuelewa na kusema kweli sielewi sheria zetu naomba somo kidogo nipate kuelewa.. Hivi Mkristu (mume) akioa na mwanamke akaitaka taraka (sheria ya nchi) kinyume cha sheria ya dini...Je, kuna uamuzi upi hapa?
 
Msekwa%2811%29.jpg

Makamu Mwenyekiti CCM Bara, Pius Msekwa

Chama cha Mapinduzi (CCM), kimesema suala la kuundwa kwa Mahakama ya Kadhi Tanzania limepatiwa ufumbuzi na serikali ya awamu ya nne baada ya kupokea ushauri wa Tume ya Kurekebisha Sheria uliotaka jambo hilo kuachwa kwa waumini wa dini ya Kislamu.

Makamu Mwenyekiti CCM Bara, Pius Msekwa, aliwaambia waandishi wa habari mjini Dodoma jana kuwa uamuzi huo umetokana na ushauri uliotolewa na Tume ya Kurekebisha Sheria iliyokuwa ikiongozwa na Jaji Ibrahimu.

Msekwa aliyeongozana na Katibu Mkuu wa CCM, Yusuf Makamba, alisema ahadi ya kuanzishwa kwa Mahakama ya Kadhi ilitolewa katika Ilani ya Uchaguzi ya chama chake ya mwaka 2005 hadi 2010 katika kifungu cha 108 (B).

Alisema kifungu hicho kinasomeka kuwa “kulipatia ufumbuzi suala la kuanzishwa kwa Mahakama ya Kadhi Tanzania Bara”

“
Baadhi ya watu hawakuelewa maana ya kifungu hicho ambacho kililenga katika kulitolea ufumbuzi suala hili na si kuunda chombo hicho,” alisema. Alisema katika kulitafutia ufumbuzi jambo hilo, CCM ililikabidhi suala hilo katika Serikali ya Muungano na serikali ililifanyia kazi kwa kutumia chombo chake cha Tume ya Kurekebisha sheria.

Alisema Serikali ikiunda mahakama hiyo itakuwa imekwenda kinyume na Katiba ya Nchi ambayo inasema serikali haina dini.

“
Lakini kwa kuwa suala hili linahusu taratibu za dini ya kiislamu, Waislamu wako huru kuunda mahakama hiyo ndani ya taratibu za dini yao na Waislamu wenyewe wameshajulishwa kuhusiana na uamuzi huu,” alisema Msekwa.

CHANZO: NIPASHE

Tunaingojea kwa hamu tuone je hao waliiomba Serikali iwape Ruhusa kuweka hiyo Mahakama je Watafuata haki kweli katika kutekeleza hizo sheria za mahakama ya Kadhi?

wasije lete sheria kama za Kisomali? Kufuga ndevu na kadhalika.
 
Bongoland,
Mkuu samahani kidogo hapa sijakuelewa na kusema kweli sielewi sheria zetu naomba somo kidogo nipate kuelewa.. Hivi Mkristu (mume) akioa na mwanamke akaitaka taraka (sheria ya nchi) kinyume cha sheria ya dini...Je, kuna uamuzi upi hapa?

sheria ya nchi itaheshimiwa na taraka itatolewa.
 
sheria ya nchi itaheshimiwa na taraka itatolewa.
Shukran, umesema Taraka itatolewa!.. Sasa kwa kufuata kifungu gani? mathlan ktk sheria ya ndoa Part 2 (Nature of Marriage)sehemu ya 11 (5) kinasema hivi:-

No marriage between two Christians which was celebrated in a church in Christian form may, for so long as both the parties continue to profess the Christian faith, be converted from monogamous to polygamous and the provisions of this section shall not apply to any such marriage, notwithstanding that the marriage was preceded or succeeded by a ceremony of marriage between the same parties in civil form or any other form.

Sasa naposoma kifungu hiki nakuta dini moja imetajwa kwa ufasaha na kwamba provisions hazita apply kwa ndoa yeyote ya aina hii.. Hapa kidogo naomba msaada ni provisions zipi hizi na kwa nini zisiwe applied ktk ndoa hii hali zitakubalika ktk ndoa nyinginezo.
 
ilimladi inaghalimiwa na waislam na haiwausu wengine kwa lolote, na hita enda kinyume na sheria mama katiba waendelee tu.
 
Shukran, umesema Taraka itatolewa!.. Sasa kwa kufuata kifungu gani? mathlan ktk sheria ya ndoa Part 2 (Nature of Marriage)sehemu ya 11 (5) kinasema hivi:-

No marriage between two Christians which was celebrated in a church in Christian form may, for so long as both the parties continue to profess the Christian faith, be converted from monogamous to polygamous and the provisions of this section shall not apply to any such marriage, notwithstanding that the marriage was preceded or succeeded by a ceremony of marriage between the same parties in civil form or any other form.

Sasa naposoma kifungu hiki nakuta dini moja imetajwa kwa ufasaha na kwamba provisions hazita apply kwa ndoa yeyote ya aina hii.. Hapa kidogo naomba msaada ni provisions zipi hizi na kwa nini zisiwe applied ktk ndoa hii hali zitakubalika ktk ndoa nyinginezo.

Mwaka huu tutawekana sawa tu Tanzania yetu sote!!!
 
Bob,

Unaweza kutupatia soft copy ya hii sheria ya ndoa...tafadhali.
 
kutokana na uelewa mdogo wa mashekh, hapo walitumiwa tu kama ngazi yakuipigia kura CCM wao na waumini wao kwa madai watapewa nafasi kuianzisha hiyo mahakama
lakini kwa mwenye uelewa mkubwa alijua tu kuwa hiyo ni geresha tu, yaani mahakama inayo husu taasisi ya dini ianzishwe vipi kwa gharama za watanzania wote kwa ujumla? huu ni wakati wa waislamu kote nchini kufikiria upya ni namna gani wao wataanzisha hiki chomb kwa gharama zao wenyewe
 
Bongoland,
Mkuu samahani kidogo hapa sijakuelewa na kusema kweli sielewi sheria zetu naomba somo kidogo nipate kuelewa.. Hivi Mkristu (mume) akioa na mwanamke akaitaka taraka (sheria ya nchi) kinyume cha sheria ya dini...Je, kuna uamuzi upi hapa?

Mathayo/ Chapter 5 17. Msidhani ya kuwa nalikuja kuitangua torati au manabii; la, sikuja kutangua, bali kutimiliza.
18. Kwa maana, amin, nawaambia ,Mpaka mbingu na nchi zitakapoondoka,yodi moja wala nukta moja ya torati haitaoondoka ,hata yote yatimie.

19. Basi mtu ye yote atakayevunja amri moja katika hizi zilizo ndogo, na kuwafundisha watu hivyo, ataitwa mdogo kabisa katika ufalme wa mbinguni; bali mtu atakayezitenda na kuzifundisha, huyo ataitwa mkubwa katika ufalme wa mbinguni.

31. Imenenwa pia, Mtu akimwacha mkewe, na ampe hati ya talaka;

32. lakini mimi nawaambia, Kila mtu amwachaye mkewe, isipokuwa kwa habari ya uasherati, amfanya kuwa mzinzi; na mtu akimwoa yule aliyeachwa, azini.

Mambo ya kuachana Sio tu kwa waislam hata kwa Wakristo yapo umesoma Mkuu hapo juu?
 
kutokana na uelewa mdogo wa mashekh, hapo walitumiwa tu kama ngazi yakuipigia kura CCM wao na waumini wao kwa madai watapewa nafasi kuianzisha hiyo mahakama
lakini kwa mwenye uelewa mkubwa alijua tu kuwa hiyo ni geresha tu, yaani mahakama inayo husu taasisi ya dini ianzishwe vipi kwa gharama za watanzania wote kwa ujumla? huu ni wakati wa waislamu kote nchini kufikiria upya ni namna gani wao wataanzisha hiki chomb kwa gharama zao wenyewe

Tambo lisilo na mashiko!!!!!!!!!!!!!!!!
 
Serikali inaacha kutafuta PESA na ku-secure future za waTz na kizazi chao cha kesho, inajiingiza kwene malumbano yasiyo na kichwa wala miguu.
 
Back
Top Bottom