[FONT=ArialMT, sans-serif]Chanzo cha habari hii inayofuatia ni Gazeti la Majira la Tarehe 25,June,2010[/FONT]
[FONT=ArialMT, sans-serif][/FONT]
[FONT=ArialMT, sans-serif]Chama cha Mapinduzi (CCM), kimesema suala la kuundwa kwa Mahakama ya Kadhi Tanzania limepatiwa ufumbuzi na serikali ya awamu ya nne baada ya kupokea ushauri wa Tume ya Kurekebisha Sheria uliotaka jambo hilo kuachwa kwa waumini wa dini ya Kislamu. Makamu Mwenyekiti CCM Bara, Pius Msekwa, aliwaambia waandishi wa habari mjini Dodoma jana kuwa uamuzi huo umetokana na ushauri uliotolewa na Tume ya Kurekebisha Sheria iliyokuwa ikiongozwa na Jaji Ibrahimu.[/FONT]
[FONT=ArialMT, sans-serif][/FONT]
[FONT=ArialMT, sans-serif]Msekwa aliyeongozana na Katibu Mkuu wa CCM, Yusuf Makamba, alisema ahadi ya kuanzishwa kwa Mahakama ya Kadhi ilitolewa katika Ilani ya Uchaguzi ya chama chake ya mwaka 2005 hadi 2010 katika kifungu cha 108 (B).[/FONT]
[FONT=ArialMT, sans-serif][/FONT]
[FONT=ArialMT, sans-serif]Alisema kifungu hicho kinasomeka kuwa kulipatia ufumbuzi suala la kuanzishwa kwa Mahakama ya Kadhi Tanzania Bara[/FONT]
[FONT=ArialMT, sans-serif]Baadhi ya watu hawakuelewa maana ya kifungu hicho ambacho kililenga katika kulitolea ufumbuzi suala hili na si kuunda chombo hicho, alisema. Alisema katika kulitafutia ufumbuzi jambo hilo, CCM ililikabidhi suala hilo katika Serikali ya Muungano na serikali ililifanyia kazi kwa kutumia chombo chake cha Tume ya Kurekebisha sheria.[/FONT]
[FONT=ArialMT, sans-serif][/FONT]
[FONT=ArialMT, sans-serif]Alisema Serikali ikiunda mahakama hiyo itakuwa imekwenda kinyume na Katiba ya Nchi ambayo inasema serikali haina dini.[/FONT]
[FONT=ArialMT, sans-serif]Lakini kwa kuwa suala hili linahusu taratibu za dini ya kiislamu, Waislamu wako huru kuunda mahakama hiyo ndani ya taratibu za dini yao na Waislamu wenyewe wameshajulishwa kuhusiana na uamuzi huu, alisema Msekwa[/FONT]
My take:
Kumbe walipoliingiza suala la Mahakama ya Kadhi kwenye Ilani yao ya Uchaguzi mwaka 2005 ilikuwa tu kuwadanganya Waislam ili wazipate kura zao?Dr Ngasongwa aliye asisi mpango mzima wa Mahakama ya Kadhi dhidi ya Jumuia za Kiislam ili tu wapate kura zao anastahili adhabu gani?
CCM wanasema Serikali imelipatia tayari ufumbuzi suala la Mahakama ya Kadhi,ni ufumbuzi gani waliwapatia wanao dai mahakama ya Kadhi ili hali haijaanzishwa?
CCM wanasema kuwa Serikali haiwezi kuisaidia dhehebu fulani kuanzisha mahakama zake;je hawakujua mapema kama mahakama ya Kadhi ni suala la kidini?Kama walijua iweje basi waliingiza kwenye Ilani yao ya Uchaguzi?
Kwa kweli JK,Msekwa,Pinda,Ngasongwa na Makamba tunataka maelezo ya kina dhidi ya jambo hili sio majibu shallow kama haya ya Mzee Msekwa!