Kipi bora kubadilisha oil kwa kuangalia muda au kwa kuzingatia mileage?

Kwa gari yenye 1000cc na kushuka chini, badili oil kila baada ya km 2000, bila kubadili oil filter. Badili oil filter kila baada ya km 4000.

Kwa gari yenye 1001cc - 1500 cc, badili oil kila baada ya km 2500, badili oil filter kila baada ya km 5,000.
Kwa gari ya 1501cc - 2500cc, badili oil kila baada ya km 3,000, badili oil filter kila baada ya km 6,000.

Kwa gari ya 3,000cc na kuendelea yenye piston sita, waweza badili oil na oil filter kila baada ya km 5000.
Hii ni kwa gari za Petrol.

Kwa gari za Diesel, waweza kubadili oil na filter kila baada ya km 5,000 kwa magari ya light duty.
Kwa heavy duty, jitahidi isizidi km 10,000 hasa kwa hizi gari za kichina. Fanya hivi ili injini ya gari yako idumu.
Kwa oil hizi hizi substandard za hapo Livingstone? 🤣 Ama kwa Oil imported from Europe?
 
Kwa experience yangu gari langu huwa nafanya kwa Km 5000 ila kwa range ya miezi 6 hata kama hazijafika huwa nafanya kwahyo me huwa nna calculate interval ya muda plus Km coz me sina mizunguko mingi na gari gari lenyewe nilinunua lina Km 44,000 mwaka 2018 na hadi leo 2023 bado lipo Km 80k
 
Mkuu hiyo gari itadumu na kwa maelezo yako tu gari yako unaithamini si tu kwenye oil hata na service nyingine
 
WATENGENEZAJI WANASHAURI KUANGALIA KM Kulingana na aina ya oili uliyoweka.

zamani oili zilidumu 3000km saivi kuna za 5000km na 10,000km
Ni kweli kabisa mkuu lakini ishu inakuja kwenye filter utakayoiweka itamudu hizo km 9000? Binafsi ntakuja na somo la filter kazi yake na umuhimu wake kwenye gari na madhara ya kuweka filter feki ambazo kwa bongo ndo zimejaa
 
Hivi unatambuaje FEKI na genuine filter?
 
Kwa gari yenye 1000cc na kushuka chini, badili oil kila baada ya km 2000, bila kubadili oil filter. Badili oil filter kila baada ya km 4000.

Kwa gari yenye 1001cc - 1500 cc, badili oil kila baada ya km 2500, badili oil filter kila baada ya km 5,000.
Kwa gari ya 1501cc - 2500cc, badili oil kila baada ya km 3,000, badili oil filter kila baada ya km 6,000.

Kwa gari ya 3,000cc na kuendelea yenye piston sita, waweza badili oil na oil filter kila baada ya km 5000.
Hii ni kwa gari za Petrol.

Kwa gari za Diesel, waweza kubadili oil na filter kila baada ya km 5,000 kwa magari ya light duty.
Kwa heavy duty, jitahidi isizidi km 10,000 hasa kwa hizi gari za kichina. Fanya hivi ili injini ya gari yako idumu.
Nashukuru sana. Nimekuja kula madini hapa. Natarajia kununua Kigari sasa naanza kuvuna akili kabla ya kumiliki 😁😁
 
Hivi unatambuaje FEKI na genuine filter?
niliwahi kukutana na hili somo tamesa kwenye naonyesho ya nane nane nyakabindi walikuwa wamezichana filta og na feki...kuna smaku chini ya filta moja ina nguvu zaidi nyingine nguvu hafifu..alafu yale makaratasi mule ndani kuna karatasi nzito na bora na kuna nyingine nyepesi kuna wavu kuna mwengine ni wavu mwepesi kama wa mbu na kuna mwengine ni bati zito liliotobolewa...kuzijua ndio mtihani ila ukienda kununua chukua sammple zilinganishe utaona utofauti
 
Back
Top Bottom