Kipi bora kubadilisha oil kwa kuangalia muda au kwa kuzingatia mileage?

Kwa oil hizi hizi substandard za hapo Livingstone? 🤣 Ama kwa Oil imported from Europe?
 
Kwa experience yangu gari langu huwa nafanya kwa Km 5000 ila kwa range ya miezi 6 hata kama hazijafika huwa nafanya kwahyo me huwa nna calculate interval ya muda plus Km coz me sina mizunguko mingi na gari gari lenyewe nilinunua lina Km 44,000 mwaka 2018 na hadi leo 2023 bado lipo Km 80k
 
Mkuu hiyo gari itadumu na kwa maelezo yako tu gari yako unaithamini si tu kwenye oil hata na service nyingine
 
WATENGENEZAJI WANASHAURI KUANGALIA KM Kulingana na aina ya oili uliyoweka.

zamani oili zilidumu 3000km saivi kuna za 5000km na 10,000km
Ni kweli kabisa mkuu lakini ishu inakuja kwenye filter utakayoiweka itamudu hizo km 9000? Binafsi ntakuja na somo la filter kazi yake na umuhimu wake kwenye gari na madhara ya kuweka filter feki ambazo kwa bongo ndo zimejaa
 
Ni kweli kabisa mkuu lakini ishu inakuja kwenye filter utakayoiweka itamudu hizo km 9000? Binafsi ntakuja na somo la filter kazi yake na umuhimu wake kwenye gari na madhara ya kuweka filter feki ambazo kwa bongo ndo zimejaa
Hivi unatambuaje FEKI na genuine filter?
 
Nashukuru sana. Nimekuja kula madini hapa. Natarajia kununua Kigari sasa naanza kuvuna akili kabla ya kumiliki 😁😁
 
Hivi unatambuaje FEKI na genuine filter?
niliwahi kukutana na hili somo tamesa kwenye naonyesho ya nane nane nyakabindi walikuwa wamezichana filta og na feki...kuna smaku chini ya filta moja ina nguvu zaidi nyingine nguvu hafifu..alafu yale makaratasi mule ndani kuna karatasi nzito na bora na kuna nyingine nyepesi kuna wavu kuna mwengine ni wavu mwepesi kama wa mbu na kuna mwengine ni bati zito liliotobolewa...kuzijua ndio mtihani ila ukienda kununua chukua sammple zilinganishe utaona utofauti
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…