Kipi bora, kuishi maisha marefu ya shida au mafupi yenye raha?

Kipi bora, kuishi maisha marefu ya shida au mafupi yenye raha?

Jplus Jr

Senior Member
Joined
Dec 29, 2018
Posts
124
Reaction score
147
Ishi maisha ya utajiri unaotokana na ushirikina hata iwe kwa masharti ya kuishi muda mfupi mfano mika 10 hadi 20 ya kula bata kwa sana. Ila baada ya hapo ufe.

Au

Uishi maisha yako kwa muda mrefu haijalishi unapitia magumu na maisha ya shida kiasi gani ila tu hauko tayari kuishi maisha ya utajiri kwa njia ya ushirikina.

Nachowaza unaweza jikuta umeteseka sana katika kipindi chako kingi cha kuishi duniani na bado ukajikuta mko njia moja katika Jehanamu kwa mjibu wa vitabu vya kiroho na yule aliyeishi maisha ya bata kupitia utajiri kwa njia ya ushirikina.

Nini maoni yako juu ya hili.
 
Hakuna maisha yasiyo na utaratibu au sheria,ogopa sana maisha ya kupangiwa na kiumbe mwenzako namna ya kuishi,kuvaa,kula,kuhusiana na watu nk.

Utajiri wa mali haujawahi kuleta suluhisho la maisha ya utoshelevu,bali hofu na mashaka ndio hutawala.

Zaidi ya 69% ya matajiri wanaishi maisha ya hofu sana kulinganisha na wasio matajiri.

Kuishi ushirikina na kukubali kuwa mtumwa. Amani ya moyo ni moja ya njia nzuri ya kufurahia maisha.

Tafuta pesa,tumia pesa,ila pesa isikufanye mwendawazimu.
 
Bora nipambane na hali yangu tu bila ushirikina, Pesa za majini zina masharti kibao siyawezi. Mara usilale kitandani mwako, mara utembee peku, mara usivae Viatu, mara usipande daladala.

Huh! Cha kufia kipi
 
Bora nipambane na hali yangu tu bila ushirikina, Pesa za majini zina masharti kibao siyawezi.. Mara usilale kitandani mwako, mara utembee peku, mara usivae Viatu, mara usipande daladala...

Huh! Cha kufia kipi
Hivi na yule rasi mpoto yumo humor?
 
Itakuwa umetoka kushawishiwa sasa upo dilema unaona uje usikilize mashauri ya sana Jf

Nakushauri tu rudi kamuulize Mzazi wako kama njia uitakayo ni sahihi

Maadamu wao ndo huwa wa kwanza kutolewa sadaka.
 
Elewa HILI Kama Kuna thawabu nyingi na kidogo alafu Kuna dhambi kubwa na kidogo

Basi kaa ukijua hata jehanam inatofautiana kulingana na kiwango Cha dhambi ulizonazo sio wote tutakuwa sehemu MOJA na waliotupa zile maiti kwenye mifuko baharini
 
Jiulize unatoka wapi!??? Unaenda wapi!??? Hapo utajua ufanye nini sasa!!!
 
Sasa kama hupandi daladala ila usafiri wako shida i wapi?
Bora nipambane na hali yangu tu bila ushirikina, Pesa za majini zina masharti kibao siyawezi. Mara usilale kitandani mwako, mara utembee peku, mara usivae Viatu, mara usipande daladala.

Huh! Cha kufia kipi
 
[emoji1787][emoji1787]
Itakuwa umetoka kushawishiwa sasa upo dilema unaona uje usikilize mashauri ya sana Jf

Nakushauri tu rudi kamuulize Mzazi wako kama njia uitakayo ni sahihi

Maadamu wao ndo huwa wa kwanza kutolewa sadaka.
 
Unamaanisha huko jehanamu kuna adhabu kubwa kubwa na ndogo ndogo mkuu?
Elewa HILI Kama Kuna thawabu nyingi na kidogo alafu Kuna dhambi kubwa na kidogo

Basi kaa ukijua hata jehanam inatofautiana kulingana na kiwango Cha dhambi ulizonazo sio wote tutakuwa sehemu MOJA na waliotupa zile maiti kwenye mifuko baharini
 
Bora nipige raha kwa sana!! then Baba Mungu tutaongea tu!! atanisikiliza shida zangu tena tutaelewana!! sisi wote ni watoto wake hata huyo shetani mnae mzodoa na kumsimanga kaumbwa na kupewa uwezo na Mungu wenu huyo huyo aliye waumba tena mwenzenu yuko mbali anamjua Mungu kuliko nyie wamatumbi!!!
 
Yaani Maisha mafupi miaka 10-20 kutokea hapa nilipo au tokea nizaliwe. Kama tokea hapa nilipo, KANYAGA TWENDE.

Unaweza jikuta unataka marefu ya msoto lakini still usi survive hiyo 10-20 kutokana na struggle za hapa na pale.

Kikubwa ni izo hela zisiwe na masharti ya Kingese.
 
Bora kuishi kama Mbuzi mwaka mmoja kuliko kuishi miaka miamoja kama Kondoo
 
Back
Top Bottom