Kipi bora kununua Hiace mpya kwa 30M ama kuchukua Tata Marcopolo kwa mkopo

Ego is the Enemy

JF-Expert Member
Joined
Mar 21, 2014
Posts
8,201
Reaction score
16,246
Habarini wanajamvi.

Ninaombeni msaada Wa kimawazo na ushauri kwa wenye uzoefu na hii biashara. IPI bora Nina 40M ninafikiria kuiwekeza kwa biashara ya huduma za usafirishahi Wa abiria.

Hapa nilipo nipo njia panda kati kununua hiace mpya inayo range 25-30M ama niende pale kwa wahindi niwape 30+M wanipe marcopolo tata mpya yenye zero mileage afu nawalipa kidogokidogo wanabaki na kadi original.

Hii inaweza ikaleta hesabu ya 200k kwa siku wakati hiace itanilazia 50k kwa siku. Hii tata mpya ninawazia mana ni mpya hivyo zile heavy services and spear replacement rate inakuwa ni ndogo kuliko hii used hiace.

Karibuni kwa wenye mawazo positives tushauriane katika kuusukuma umasikini mbali.
 
Chukua hiyo ya kulaza 200k kwa siku ukipiga mwezi una milioni 6,
Ndani ya miezi sita ukitoa service ndogo ndogo unamaliza deni na kuanza kula faida,

Nb.
Kuwekeza kwenye biashara ya Usafiri kunahitaji Uvumilivu na kujitoa maana muda wowote kitu kikibuma/mnemba unapata lose.
 
Ila niongezee hapo bro nadhani kama kuna option ya Eicher ni nzuri zaidi kwa mawazo yangu
Thank you mkuu ubarikiwe. Unaweza ukanipa muda wako kwa kuweka nyama kidogo ni kwa sababu gani na wengine ili tujifunze kwa kuelezea tofauti ya tata na eicher. Nina imani tumezaliwa hata hatuwajui wazazi ila tumekuwa wakubwa tukawajua. Am sure everything is learnable kikubwa uwe tayari kujifunza
 
Nakushauri kwa uzoefu, nimetoka Kahama kumpelekea MTU Coaster 24 namba DE ambayo tumnunulia kwa 36m. Nakushauri nunua Coaster iliyo kwenye hili nzuri, itakulipa.

Wakati narudi nikakosa usafiri wa Trinity ya Rwanda, nikapata Coaster ya kampuni ya Travel Partner jamaa ametujaza utadhani machungwa. Nikawaza kuwa kumbe MTU unaweza kuanzisha route ya mchana na ikakulipa sana! Maana Kahama To Dar mafuta hayazidi laki tano na wasafiri wapo!

Wakati tunaondoka juzi tulipata abiria wengi tu njiani na tuliondoka Dar SAA Tisa mchana jumapili!


So kuna fursa kwa kweli. All the best
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…