Kipi bora kununua incubator au kuanza nae kuku wa kienyeji 40?

Sinaharaka mkuu ilimradi kitu nnachokifanya ni sahihi basi nipo na uvumilivu wakutosha tu
Kama una haraka! Ingia kijijini chukua kuku 20 kwanza uone! ila kuwa muangalifu yaani uwe unawasoma muda wote na uwe na elimu ya kuchagua kuku..
 
Mkuu anza na incubator uwe tayari kulea vifaranga

Ukitotoa unalea na mteja akija akitaka umri wowote unauza

Pia unaweza ukakodiswa kutotolesha ukalipwa kulingana na idadi ya mayaiView attachment 1101178
Mkuu nimevutiwa na ubunifu wako, nami nipo mbioni kutengeneza yangu, shida inakuja kwenye hivyo vifaa vya kupimiA joto, vp hivyo vifaa ulinunua bei gani na vinapatikana wapi??
 
Mkuu nimevutiwa na ubunifu wako, nami nipo mbioni kutengeneza yangu, shida inakuja kwenye hivyo vifaa vya kupimiA joto, vp hivyo vifaa ulinunua bei gani na vinapatikana wapi??
Mkuu nipo Kilimanjaro kama unahitaji vifaa ni pm nikupatie digital temprature controla hiyo inayo onesha namba hapo kwenye picha hicho kifaa kinakuonyesha kiwango cha joto na kama joto likizidi hupooza ili mayai yasiungue karibu mkuu
 
Yes mkuu maana najua taratibu ntaongeza Mtaji na kwakuanza na kuku 100 sio mbaya
Usianze na kuku 100.anza na kuku wachache wa zaliane wenyewe na kufikia idadi hio, anza hata 30.Maisha hayataki haraka utafeli vibaya.
 
Anza na Kuku wakubwa 40 kuntunza vivaranga ni gharama kubwa sana mkuu na bado hawajafa.
 
Mkuu naweza pata ya mayai 30 kwa sh ngap
Mkuu jamaa ametengeneza mwenyewe and nadhan ukimuomba akuelekeze atakuelekeza vzuri.... Mm mwenyewe nimeiunda ya kwangu nasubiri matokeo tu
 
Achaneni na hii biashara utali mbele ya safari. Model ya Biashara za kuangulisha ni ngumu sana.

Watu wengi kwa sasa wamefungia incubator ndani nikiwemo mimi.

Shida ni Model ya hii biashara sio rafiki kabisa kwa Watu wadogo
 
Sio rahisi kihivyo. Hii biashara ina Chalnge kubwa mno hasa Stracture ya biashara.

Hii Model ina wafaa sana wenye mitaji mikubwa kama wakina Interchick ma kadhalika

Mkuu Mimi naona bora kununua incubator, kwani Licha ya gharama, ukiitunza vizuri itadumu muda mrefu, na utatimia Kama ajira kuwauzia watu vifaranga au nimekosea mkuu?
 
Kuku wa Kienyeji kwanza Tambua sio kuku wa biashara.

Kuku wa biashara ni Layers na Broiler pekee.

Kuku wa kienyeji sio kuku wa kufuga kibiashara wale labda huko vijijini watu wanajifugia tu ila wana mambo mengine.

Kama unataka kufuga Fuga Layers na Broiler.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…