Kipi bora: Kuoga Usiku au Asubuhi?

Kipi bora: Kuoga Usiku au Asubuhi?

BM X6

JF-Expert Member
Joined
Nov 24, 2020
Posts
1,376
Reaction score
4,222
Wote tunajua umuhimu wa kuoga na kila mtu ana ratiba yake ya kuoga ukiachana na wale wanaooga mara mbili kwa siku Kuna sisi ambao kuoga kwetu ni mara moja tu kwa siku, so ni kuchagua tu mwenyewe uoge Asubuhi au Usiku

Binafsi napenda kuoga Asubuhi mara nyingi, ni mara chache sana naweza kuoga usiku tena ikitokea siku nimeoga usiku basi kesho Asubuhi nitajisikia uvivu kuoga tena

KWANINI NAOGA ASUBUHI?

Naoga Asubuhi kwasababu naamini ndio muda sahihi wa kutoa uchafu wote ikiwemo na seli za ngozi zilizokufa and other bodily fluids

Pia nakua fresh zaidi kuianza siku mpya

KWANINI SIOGI USIKU

Mwili wa mwanadamu bado huwa unazalisha harufu mbaya usiku na hukusanya wadudu na seli za ngozi zilizokufa. hivyo kama Ukioga usiku itakulazimu kuoga tena Asubuhi kitu ambacho ni Anasa na upotevu wa Maji

Kwako kipi Bora na Sahihi? Kuoga Usiku au Asubuhi? Uzi unawahusu Wanaume tu, Wanawake Najua ni muhimu kuoga mara 2 Kila siku
Screenshot_20220618-121553.jpg
 
Mimi naona asubuhi ili kuchangamsha akili ifanye kazi sawasawa katika uzalishaji mali.

Usiku ukiwa umechoka uchovu unaweza kukufanya unalala vizuri tu sema inategemea na kazi ulizofanya kutwa nzima na kama mchangoaji mwingine alivyosema iwapo umeoa au kuolewa!
 
Wanawake kuoga ni lazima...
Wanaume kuoga ni hiari...
[emoji23]
Uwe mwanamke, uwe mwanaume, ukiwa sehemu yenye joto kama Dar itakubidi kuoga at least mara 2 kwa siku, unapoamka na unapokwenda kulala.

Utalalaje bila kuoga wakati joto ni kali na unatoa jasho kama umemwagiwa maji? Kwa sehemu nyingine zenye baridi, kwa mwanaume unaweza kuoga mara moja kwa siku kulingana na kazi unayofanya.

Kuna kazi za kwenye mavumbi na kutoa jasho kwa mfano.
 
Si tulikubaliana kwamba hili jiji lina joto kwa sie ambao hatuna pesa mkuu, wenzetu wanaokaa mbweni na viunga vyake Wanachezea kipupwe tu, hilo joto watakutana nalo wapi?
 
Si tulikubaliana kwamba hili jiji lina joto kwa sie ambao hatuna pesa mkuu, wenzetu wanaokaa mbweni na viunga vyake Wanachezea kipupwe tu, hilo joto watakutana nalo wapi?
Ni kweli. Hata usafiri wanakuwa kwenye madude yenye aircondition kali. Hotel wanazokwenda nazo hivyo hivyo.
 
Back
Top Bottom