Kipi bora kuuza mali zako kumsomesha mtoto ili aje akusaidie baadae au ubaki na mali zako na mtoto umpa elimu ya maisha

Hemedy Jr Junior

JF-Expert Member
Joined
Feb 17, 2023
Posts
915
Reaction score
1,082
Familia nyingi zimefeli baada ya kumaliza mali kama mashamba,mifugo n.k kwa kuwasomesha watoto wao mwisho watoto wao wamekuja na vyeti nyumbani.

Elimu ya maisha yamekosa hata elimu waliyoipata huko shuleni wamerudi mtaani haitumiki.

elimu yako ndo inayokutesa.... kazi unayofanya sasa hivi ndo hiyo hiyo ulosomea? Au umejiongeza
 

Zaa watoto wachache na miliki Mali nyingi Hakikisha mtoto Hapatikani katika haya makundi akiwa na umri wa 12-40

Mlevi
mzinifu
shoga/msagaji
Mchawi/Mlozi
 
Si bora hao wanao kuja na vyeti mkuu wenda siku moja CCM itawakumbuka angalau iwape kibarua cha mshahara wa 500,000 kwa mwezi.
,Wengine wanakuja na mimba na kukupa mzigo mwingine wa kulea wajukuu wakati wamesha kufirisi ,wao wanasepa zao mjini kudanga.

Dah wazazi wa kizazi hichi mna kazi sana,ila mmeyataka wenyewe kwa kujitia eti mnalea watoto wenu kizungu.
 
Kumsomesha mtoto sio fadhila lakin. Kwamba uje kulipwa baadae. Kusomesha ni wajibu. Ukiweza somesha sana tena shule ya bei ghali unavyoweza lakin usisahau kutafuta maisha yako binafsi na kuhakikisha unaacha alama hapa duniani. Wasaidie kadiri inavyowezekana wasiojiweza hasa watoto yatima kuwasaidia kusoma maana baada ya kupata pesa hakuna jipya Zaid ya kuona faraja watu uliowasaidia.
 
Baki na Mali zako ,mpeleke mtoto shule za kawaida tu ,huku ukimfundisha jinsi ya kupambana na maisha .

Huko mbeleni watu waliosoma sana ndio watakua na maisha magumu ,maana wengi hawajui jinsi ya kupambana na maisha wanategemea vyeti viwabebe huku ajira zenyewe hakuna , wengi wao hawawezi kufanya kazi za kawaida Kwa mfano biashara za uchuuzi wakiamini hizo hufanya watu ambao hawajasoma , kumbe kupitia hizo hizo biashara wenzao wanatoboa tu .
Pia Kuna wengine wamesomeshwa na hizo hizo biashara ndogo ndogo .

Nakazia tuwafundishe watoto jinsi ya kupambana na maisha
 
Shukhuran 🙏 mesej imefika
 
Jamii za wakulima na wafugaji kijana anazaliwa kwenye mifugo anachunga mifugo anashiriki uzalishaji Mali katika familia Kama kilimo nk akifikisha umri wa kuoa anatafutiwa mke anaozeshwa, anapewa eneo anajenga anapewa mifugo kadhaa anapewa mashamba kijana anakomaa na mifugo na kilimo baada ya maiaka minne uyu kijana anakuwa na ukwasi wa kutosha mifugo kibao uyu kijana ajui kusoma Wala kuandika


MY TAKE
Kama una uwezo wakutafuta Mali tafuta Mali Yani tafuta jenga, miliki aridhi nk wanao watavikuta wakichezea atatukuta walimwengu tutamfunza
 
Bongo kuwa na elimu ni sawa kupata kaz n bahat
Na ukipata kazi ya kupata kaz nzur serikalin utabaki kubadirishwa idara ata ungekuwa na miaka 79 ndo maana kaz imekuwa kazi kuipata ko bongo tunabahatisha tu kat ya elimu na kaz

Amuwa mwenyew apo
 
Mbona tunaongelea negative tu kwani hakuna waliosomeshwa kwa njia hizo na wakapata kazi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…