Kipi bora kuuza nyumba au kufanya dhmana ya mkopo?

GAZETI

JF-Expert Member
Joined
Feb 24, 2011
Posts
5,286
Reaction score
6,736
Nimeamua tu kuwashirikisha baada ya kuombwa ushauri, kwa upande wangu ni sahihi kabisa
na wala sina hofu kabisa juu ya hilo.

Jamaa mambo yamembana sana hana kazi kwa sasa, kifupi ameyumba sana kimaisha.
Tayari ameshampata mteja anayehitaji nyumba yake kwa milioni 75 kutokana na ubora
wa eneo ilipo hiyo nyumba.

Wengi wanamshauri asiuze, binafsi naona woga wa kuuza nyumba hauna maana kabisa
auze kisha anunue nyumba ya nafuu maisha yaendelee.

Vipi mwana JF nipe mtazamo wako kipi bora kuuza au kutumia kama dhamana ya mkopo?
 

Tatizo unaweza kumshauri kuuza kwa hiyo mil 75 wakati tayari ana commitment na madeni ya zaidi ya mil 30 tayari..hapo piga hesabu atabakiwa na sh ngapi? Ukitazama hiyo 75 unaweza kuiona nyingi kumbe kiu halisia ana mil 20 tu hapo..ni hatari kumshauri mtu aliyefirisika na ana stress kuuza asset kama nyumba!!.. utamtia shimoni zaidi..msilazimishe kuishi kama zamani ugumu wa maisha kwa sasa hauepukiki na upo kwa watu wengi na usiwafanye mkapoteza assets zenu kwa kulazimisha ku mantain maisha kama ya zamani
 
Tunajua nyumba 75m. Je anadaiwa kiasi gani?
 
Kuifanya dhamana

the great
 
Kama thamani ya hiyo nyumba ni 75m, benki itamkopesha 35m tu. Akishindwa marejesho nyumba inaondoka kwa nusu bei.
 
...sasa kama kishapata mteja si kashaamua kuuza?
..wanaomshauri asiuze waache kiherehere!
 
Huyo ni ww usizuge apa..na unauza ukaonge manzi[emoji13] [emoji13] [emoji13] [emoji13] [emoji86]
πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€
 
Usawa huu kuuza nyumba ni hatari zaidi ya gaidi anayejiripua na kujitoa mhanga kwa mabomu.

Mkuu, nyumba ndiyo uhai. Ukiuza tu kaburi linakuita.

Ngoja wengine nao watoe nasaha zao, nitarudi tena.
 
Sawa kabisa lakini kwa mtu ambaye anajitambua mil 20 unaweza kusimama nayo
vema na ukarudi kwenye nafasi yako ya awali
 
Usawa huu kuuza nyumba ni hatari zaidi ya gaidi anayejiripua na kujitoa mhanga kwa mabomu.

Mkuu, nyumba ndiyo uhai. Ukiuza tu kaburi linakuita.

Ngoja wengine nao watoe nasaha zao, nitarudi tena.
Unauza tu mkuu ili upate mtaji.
 
Sawa kabisa lakini kwa mtu ambaye anajitambua mil 20 unaweza kusimama nayo
vema na ukarudi kwenye nafasi yako ya awali


Kumbe wewe umeisha fanya maamuzi ya kuiza nyumba.

Basi, endelea vivyo hivyo utarudi hapa ukichana mdomo kama mamba.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…