Kipi bora kuuza nyumba au kufanya dhmana ya mkopo?

Nyumba ni asset, asseti ni kitu kinachogenerate income.kama hiyo nyumba iko oversize kwake auze aje huku msongola kwetu anapata ya mil 15 halafu anaanza mishe upya.kama ni mchaga atarudi kwenye reli
Ila kama ndiyo wale wenzangu wa mpe mruke hapo atakuwa amesha jichimbia kaburi.maana atataka auze nyumba ila aendelee kuishi sinza kwa kupanga
 
Umenena mkuu kuuza asset alafu huna hata ujuzi wowote wa biashara ndo unakuwa maskini kabisa.bora ajipange kivingine sio kuuza asset.
 
nyumba ni asset muhimu sana... ila sio sahihi unakaa nyumba kali huku huna hata ela ya kula au watoto hawana ada..

kama mwanaume kamili aliyejenga nyumba kwa jasho lake na anapitia wakati mgumu ni bora akauza nyumba yake hiyo milion 75... milion 3 mpaka 5 akanunua kiwanja popote pale.. akajenga low cost house isiyoidi milion 20... akaamia na familia yake...

kisha milion 40 acheze nayo kwenye biashara anayotaka kufanya kwa umakini sana...

na milion 10 ifanye majukumu muhimu ya kifamilia ikate bima ya afya ili kuondoa gharama za matibaby za familia kwa hela yake ya biashara...

pia asicheke na ndugu yeyote hata harusi asichangie kabisaaaa... a cut cost zote yaani hela ya kuuza nyumba aione kama amekopa vile....

nina imani akiizungusha vizuri atajenga nyumba ingine zaidi ya ile ya zamani.....

kukopea benki sio sahihi maana benk watampa hela ndogo sana huwa hazifati thamani ya nyumba sana.. nyumba hiyo ya 75 benk wanaweza kupa milion 35 tu.... na usipolipa nyumba wanauza tu
 
Yuko mzee mmoja msaafu alikuwa Dereva serikalini, aliuza nyumba akanunua gari
baadae akajenga tena.


Kila Heri.

Ila kumbuka, usitembelee nyota ya wenzio!

Maana , mwisho wa siku utaangukia pua itatoboke matundu 20+ utashindwa tundu za pua ni zipi zinatumika wakati wa kuvuta na kutoa hewa.
 
Kumbe hana chochote kabisa isipokuwa huyo nyumba ya 75m? na hawezi kupata kazi kabisa? kwa nini asikodishe nyumba hiyo achukue kodi maisha yaendelee?

Your great in you're up stairs.
I wish to meet you!!!
 
Hujatoa ushauri mkuu,kwa upande wangu mwambie auze nyumbe.
House is an liability

great thinker
 
Mfanyabiahsra makini hawekezi hela yake mwenyewe, anakopa, anarudisha riba..riba zipo low as much as 14% p.a
Benki gani Tz wanatoa riba 14%? Nyingi ni 18-22%. Sasa ukope hela ufanye biashara upate faida na 22% extra ya kurudisha benki lazima upate faida % kubwa sana.
 
Hivi benki huwa wanatoa mkopo bila ya kuona mtiririko wa kifedha jatika biashara yako,hapa ninamaanisha kwamba inawezekana ukapata mkopo sababu tu una asset ya kuweka dhamana wakati huna biashara yoyote inayo run?
 
Kwa ushuri mwambieni auze nyumba anunue nyumba ya sh ml 30 atapata zingine afanye mzunguko WA kibiashara ila manzi aachane nao kabisa
 
Yote yanawezekana na kila moja linaweza kua na tija, la msingi na muhimu ni kujua anachotaka kufanya baada ya kupata hiyo cash, je kina tija!?, yeye binafsi ana uwezo wa ku manage hela!?, yuko determined kwenye biashara!?, plans zake zikoje zina reflect implimintation yenye faida!? Etc , wapo watu waliopewa bilion na wakamaliza hadi 0,na wapo wenye 0 wakasimama mpaka wana bilion

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Auze nyumba upesi sana kabla kabla huyo mteja hajaghairi. Kutegemea na Umri wake., akiweka nusu ya hiyo pesa kwenye long term investment tools kama FD au hata government bonds, hata kosa laki 3-5 ya kula kila mwezi, na pesa yake itakuwa inaongezeka kupitia compound interest.

Kwa hiyo pesa Asifanye biashara kabisa. itakwisha. Anunue shamba ajenge nyumba ndogo ya byumba 2-3 alime., ila kama chekibobu, anataka kubaki mjini basi apange nyumba ya bei nafuu isiyozidi laki moja kwa mwezi.

ofcourse huu ushauri ni kwa kuzingatia kuwa mhusika hana familia kubwa inayomtegemea, watoto wanaohitaji ada n.k.

kama anafamilia, then still auze nyumba, ahamia nje ya mji kwa kununua nyumba ya gharama nafuu.,huku akiendelea kutafuta shughuli ya kufanya.lakini ahakikishe zaidi ya nusu ya hiyo pesa haitumii kwa sababu yoyote ile. in 5-10 years kwenye long terms investment facilities atakuwa na pesa zaidi ya hiyo milioni 75.
 
Hujatoa ushauri mkuu,kwa upande wangu mwambie auze nyumbe.
House is an liability

great thinker

Mbona nimetoa ushauri??..sema unapingana na mawazo yako..mimi nimeshauri asiuze sababu nyumba ni asset wewe unasema auze sababu ni liability!!..mi naona wote tumeshauri!!..
 
Aiuze aanze upya stress za kudaiwa kukomboa nyumba si poa
 
....Ana Familia, Mke na Watoto ? - Asiuze...
...Hana Familia ? - Auze, ajaribu Mambo mengine !!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…