bank ukiweka 1m ukikaa mwaka utakuta laki 8 makato kila mwezi!viwanja mkuu hata magari hayana maana
Ya Kaizari mwachie KaizariKitu ambacho ni bora zaidi ni kuwekeza fedha zako katika sehemu ambapo nondo na kutu haviharibu, wala wevi hawavunji. Na sehemu hiyo si nyingine isipokuwa ni Mbinguni alipo MFALME WA WAFALME NA BWANA WA MABWANA.
Heshima kwenu wakuu wangu.
Wakuu naombeni maoni yenu.
Kwa mfano mtu una pesa ambazo utahitaji kuzifanyia jambo fulani miaka mitano ijayo.
Kwa kawaida watu huifadhi pesa bank ila nimefikiria nikaona kwamba say una 50,000 leo,ukiziweka bank baada ya miaka mitano hata kama zitaongezeka,zitaongezeka kidogo sana.
Pia baada ya miaka mitano kitu ambacho unaweza kukifanya kwa 50,000 leo hutaweza kukifanya kwa pesa hizo hizo miaka mitano ijayo,namaanisha thamani ya pesa yetu inapungua kwa kasi sana.
Je badala ya kuziweka 50,000 zangu bank niamue kununua viwanja katika maeneo ambayo najua wakati wowote naweza kuviuza viwanja hivyo na kupata pesa zangu.
Nimeona faida ya kuziweka pesa zangu kwenye viwanja itakua ni;
Bei ya ardhi inapanda kila siku,kama leo nitanunua kiwanja kwa elfu ishirini kwa mfano,miaka mitano ijayo naweza nikakiuza kwa elfu thelathini na tano au zaidi.
Pia nitauza kiwanja kulingana na thamani ya pesa ilivyo katika miaka hiyo.
Haya ni mawazo yangu tu ila sina utaalamu katika haya ninayofikiria,hivyo ningeomba mnaojua kwa uhakika mambo haya mniambie kama mawazo yangu ni sahihi au ninakosea.
Natanguliza shukrani.
Mkuu wangu pmwasyoke nilikusudia iwe hivyo hivyo kama mfano tu.
Ningeweka kiasi halisi labda ningeonekana nina lengo la ku-show off na watu wengine wangeishia kudhihaki badala ya kunipa ushauri.
Kujishusha mara nyingi ni kuzuri.
dada QK..nakubaliana na mawazo ya baadhi ya watu wengi kuinvest hela kwenye viwanja, ila kwa mtazamo wangu kulingana na hali zetu kiuchumi ukichukulia kwamba tunapata fursa za kupata mapato mara kwa mara lakini si kwa kiasi kikubwa kwa mkupuo mmoja kama walalaheri (mfano unaweza kujikuta unaweza kuingiza au kupata Tsh 10,000 kila siku lakini ukashindwa kupata hela kubwa kwa siku moja kwa njia hizo hizo).. Hivyo kwa ushauri wangu naona ni heri (kwa kuanzia) kuwekeza katika vyama, taasisi na makampuni ya kuweka na kukopa ili baada ya hiyo miaka mitano kwa mfano utajikuta una amana (akiba) ya kiasi kikubwa sana na utakuwa na fursa nzuri ya kuwezeshwa kupata mikopo mikubwa si tu katika taasisi uliyoweka bali hata katika banki na taasisi nyingine kubwa kwa kuwa utakuwa na historia nzuri ya kuweka, tena siku hizi teknolojia imekuwa kiasi kwamba unaweza kuweka amana zako kupitia simu za mikononi....
Kwangu mimi, ni bora kufanya biashara endelevu tofauti tofauti kwa hela unazopata kuliko kununua viwanja na kusubiri viongezeke thamani.
Nimesoma comments za wadau hapa lakini bado swali moja la msingi sijaona linajadiliwa. Wewe ni mfanyabiashara? Na ni mfanyabiashara kwenye sector gani, land?
Cardinala rule number one kwenye biashara ni liquidity. Investment utakazokuwa nazo basi ni vema utilie maanani 'liquidity'. Ardhi zinapanda bei, but how long it takes turn land into cash kama uko kwenye biashara? And can that business wait mpaka uuze hiyo land na ku-inject cash?
Cardinal rule number 2, dont put all your eggs in a single basket. Ardhi zinapanda bei, vipi kama haikupanda kama ulivyotarajia? diversify your investment vinginevyo unaweza kujikuta unakula hasara.
Asante mkuu wangu kwa ushauri na ufafanuzi mzuri.
Nadhani hapa hamjanielewa,kama biashara tayari ninafanya,hizi pesa ninazungumzia shida yangu sio kuzifanyia biashara nipate faida,shida yangu ni kuzihifadhi bila thamani yake kupungua.Sihitaji biashara nyingi nyingi maana akili na nguvu zangu naelekeza kwenye biashara niliyonayo sasa ili iweze kufikia levels ninazo dream.Ubarikiwe mkuu.
Naamini nimekuelewa,
yaani unataka kukusanya fedha kwa malengo fulani huko mbele kwa namna ambayo hela hizo ziwe ktk upande ambao zinajiongeza thamani bila wewe kupata presha kubwa sana, kwa hiyo njia mojawapo uliyochagua ili kufikia lengo ni kuweka ktk ardhi ukiamini kuwa huko hela zako zitakuwa salama na zikijiongeza ( ww hutajali rate ya kujiongeza bora ziwe salama na wakati ukifika uzipate) na sio biashara.
Hivi ndivyo nilivyomwelewa mimi huyu mdada.
Asante mkuu wangu kwa ushauri na ufafanuzi mzuri.
Nadhani hapa hamjanielewa,kama biashara tayari ninafanya,hizi pesa ninazungumzia shida yangu sio kuzifanyia biashara nipate faida,shida yangu ni kuzihifadhi bila thamani yake kupungua.Sihitaji biashara nyingi nyingi maana akili na nguvu zangu naelekeza kwenye biashara niliyonayo sasa ili iweze kufikia levels ninazo dream.Ubarikiwe mkuu.
bank ukiweka 1m ukikaa mwaka utakuta laki 8 makato kila mwezi!viwanja mkuu hata magari hayana maana
Asante kwa kunielewa mkuu.
Kwa kufafanua zaidi ni kwamba,kwenye ardhi zitakua salama na pia siku yakuuza ili nipate pesa yangu,nitauza kulingana na thamani ya pesa ilivyo kwa wakati huo lakini zingekua bank thamani yake ingepungua.Kiufupi niseme kinachonifanya nisiweke bank ni kuogopa kuwa zitapungua thamani.
Ubarikiwe mkuu Malila.
mmh, bank gani hiyo mkuu ukiweka 1m unapata laki 8 kwa mwaka??