Kipi bora... Kuweka pesa Bank au kuwekeza kwenye viwanja

Kipi bora... Kuweka pesa Bank au kuwekeza kwenye viwanja

Asante kwa kunielewa mkuu.
Kwa kufafanua zaidi ni kwamba,kwenye ardhi zitakua salama na pia siku yakuuza ili nipate pesa yangu,nitauza kulingana na thamani ya pesa ilivyo kwa wakati huo lakini zingekua bank thamani yake ingepungua.Kiufupi niseme kinachonifanya nisiweke bank ni kuogopa kuwa zitapungua thamani.
Ubarikiwe mkuu Malila.

ila sasa, unaweza usizipate pesa zako kwa muda utakaoutaka! Fikiria hadi upate mteja na afike bei..!
 
Last edited by a moderator:
ila sasa, unaweza usizipate pesa zako kwa muda utakaoutaka! Fikiria hadi upate mteja na afike bei..!

ni kweli Husninyo,ila kuna maeneo mtu ukiwa nayo uhakika wa kuuza ni mkubwa.
Pia kwa kuwa tayari najua ni lini nitazihitaji hizo pesa nitakachofanya ni kutafuta mteja mapema kidogo badala ya kusubiri hadi wakati wa kuzihitaji ufike kabisa.
 
Last edited by a moderator:
kama una uwezo wa kuwa na viwanja vilivyopo kwenye maeneo mazuri, ukiwa mmiliki halali, inalipa zaidi kuliko kuweka fedha benki
 
kuweka fedha bank labda uwe na mahela mengi na uweke kwenye fixed account lakini kama ni vijisenti vya kudunduliza aisee angalia usije ukapata frustration maana bank huwa wanakata kila mwezi! ni bora ku-invest hela yako katika mradi ambao umeufanyia tathmini ya kutosha. pia kuwa makini maana biashara ziko dynamic...zinabadirika, na wewe unatakiwa uwe dynamic unapofanya biashara / investment!
 
Nami ninashukuru kwa watu wote waliotoa maoni,nami nimejifunza mengi sana kuhusu hii topic,
 
Back
Top Bottom