Kipi Bora? "Ubaya ulipwe na Ubaya" au "Ubaya ulipwe na wema"

Kipi Bora? "Ubaya ulipwe na Ubaya" au "Ubaya ulipwe na wema"

TozzyMay

JF-Expert Member
Joined
Dec 30, 2023
Posts
482
Reaction score
1,787
Haya mambo yanachanganya sana. Mtu anakufanyia ubaya halafu bado anakutaka radhi. Muda mwingine kosa lenyewe sio kosa linalotokea Kwa hatua Moja, unakuta Hadi kosa linalotokea limepita hatua kama tatu.

Sawa, unaamua kusamehe na kusema naachilia yapite , kosa linakuja linajirudia Tena ukipiga mahesabu unaona kosa kama lilianza Muda mrefu Hadi likatokea Tena, unaona kama hakustahili msamaha wa awali, unashauriwa usamehe Tena, "Ubaya ulipwe na wema"

Hapa napata swali hivi "ujinga ni Nini?"

Mtu mwingine anakukosea ,anajua kama amekukosea anaendelea na ishu zake , hajali chochote kama kakukosea. Na wewe unapotezea unasamehe kimya kimya yanaisha. Maisha yanasonga mbele ,makosa yanajirudia Tena?

Hii ndiyo inapelekea mtu mwingine kuthibitisha kwenye kila maamuzi yake "ubaya ulipwe na Ubaya" 'wema ulipwe na wema'.

Kipi Bora sasa ' kusamehe au kulipa kisasi? ' Hii inachanganya sana.
 
Ubaya kwa ubaya, wema kwa wema. HILO NDILO JIBU
Wema Kwa wema Haina ubaya,
Ubaya Kwa ubaya, maana Kuna ubaya mwingine wa tatu, unakuja. Kutoka Kwa jamaa za yule uliyemlipa ubaya . Ubaya utakuwa ubaya Hadi Tena na tenq. Amani itakwepo kweli Kwa upande wako binafsi? Baada ya kulipa ubaya?
 
Nasema hivi, kwa dunia ya sawa no ubaya kwa ubaya na wema kwa wema so chagua vinginevyo
 
Back
Top Bottom