Sidhani kama JF itakuja kuwa na GREAT THINKERS kama inavyojitangaza, kama wapo basi ni wachache sana na hawawezi kutandaza upeo na weledi wao kwenye haya majukwaa, hususani hili la elimu, wengi tunajazana jukwaa la siasa, maana humu vikinda vinaleta kero kwa kujaza mada zisizo na tija.
Mleta mada amebandika bandiko (thread) ambayo kimsingi haijitoshelezi kuweza kujadiliwa, lakini nimeshangaa kuona wachangiaji wamekurupuka kuanza kutoa michango HAFIFU ambayo kimsingi haiakisi maudhui ya mtoa mada.
Kwa hali isiyo ya kawaida, mtoa mada anadai yeye ni muhitimu wa kidato cha 6, na anahitaji ushauri chuo gani bora hapa nchini, HAMJIULIZI SWALI HAPA? kuna taarifa za msingi hazijawekwa hapa, inapaswa mtoa mada ajipange upya na arudi na taarifa toshelezi ili apewe ushauri fasaha.