Kipi hasa kiliikumba SS Ourang Medan

Kipi hasa kiliikumba SS Ourang Medan

zitto junior

JF-Expert Member
Joined
Oct 7, 2013
Posts
20,537
Reaction score
31,729
Habari za mchana wana JF natumaini kila mmoja wetu ana jumapili njema, hivyo basi moja kwa moja niingie kwenye mada husika ya leo.
images (41).jpg


UTANGULIZI
SS Ourang medan ilikuwa ni jina la meli ya huko indonesia ambayo kwa tafsiri ya jina hilo ''ourang'' yaani MTU na medan ni MJI mmoja mkubwa ulikuwa huko indonesia hivyo jina lake ni ''MTU kutoka MEDAN''. kulingana na taarifa zilizopo meli hii ilikuwa ikifanya safari zake katika mwembamba (strait) ya Malacca inayotenganisha malaysia na indonesia mwaka mpka kufikia 1947.

TUKIO
Kulingana na ripoti ya meli mbili za kimarekani yaani silver star na city of baltimore zilipata signal/taarifa za kushangaza kutoka meli hiyo ya ss ourang medan. Taarifa hyo ilisema kwa mshangao mkubwa kwamba kuna hatari kwenye meli yao,watu wanakufa kila mahala!! Na baada ya hapo kukawa na ukimya kidogo alafu huyo mtoa taarifa akaashiria naye anakata Roho.... basi mchezo ukaishia hapo na hawakupata taarifa yeyote tena.

UTAFUTAJI
Meli hyo ya silver star ikabidi iitafute ilipo ss ourang medan na baada ya vuta nikuvute wakaiona na walipofika wakakuta hakuna uharibifu wowote kwenye meli wala kiashiria cha ajali ila wakakutana na maiti tupu zimezagaa na cha kushangaza hazikuwa na dalili yeyote ya majeraha ila kilichowashtusha mabaharia hao ni kuona miili hiyo imekufa huku ikiwa na viashiri vya hofu na mshangao mkubwa mfano wengi walikuta wametoa sana macho ikimaanisha walikuwa kama na butwaa hivi na uoga, pia miili mingine ilikuwa inanyoosha mkono kwenye kitu, wengine kujificha uso kama vile wanaogopa kuangalia kitu na pozi za kufanana na hizo ila kwakuwa hakuna aliyepona wala makovu wakashindwa kupata taarifa ya nni hasa kimetokea
images (43).jpg


Huku bado wakijiuliza na kuhamaki nini kimetokea; inadaiwa kwamba moshi ulianza kufuka kutoka eneo la kuweka mizigo na wale silver star wakaamua kuitelekeza meli hiyo na kabla hawajaokoa chochote au kupata chanzo cha vifo meli hiyo taratibu ikashika moto na kuungua hadi kuzama baada ya milipuko kadhaa kwenye mifumo yake.

NADHARIA
1. Kuna baadhi ya wataalamu wanadai huenda kulikuwa na kemikali hatarishi wamebeba ila hazikufungwa vizuri hivyo zilivuja na kuwamaliza na pia wakadai moto huenda ulisababishwa na gesi hizo hizo kureact baada ya kuvuja hivyo kusababisha vifo na meli kulipuka.

Dai hili lilisema meli ilikua haijasajiliwa kokote huko uholanzi ama Indonesia ikimaanisha ilikuwa ya magendo hivyo kuna uwezekano ilikuwa inabeba silaha hatarishi ama chemical hatari kutoka Japan kupeleka costa rica baada ya vita kuu ya pili ya dunia. Ingawa dai hili linapingwa maana wanadai mabaharia wa silverstar hawakuona viashiria vyovyote vya kuvuja kwa chemical hatari ama kupanda kwa radiation levels kwenye meli.

2. Wengine (isomeke wengi) wanadai kuna tukio lisiloeleweka lilitokea kwenye meli hii, muandishi maarufu wa UFO na conspiracy theories bwana morris jessup (mwandishi wa Philadelphia experiment) naye alitoa chapisho kudai huenda viumbe wa kutoka sayari zingine Aliens walivamia meli hiyo, wengine wakadai ni majini au viumbe wa baharini, wengine wakadai walitokewa na vitu visivyoeleweka vya kiroho n.k ila mpaka sasa hakuna dai kati ya haya ambalo limethibitishwa.
images (47).jpg


UTATA
kinachoifanya tukio hili kukosa majibu mpaka leo ni fact kwamba meli hii haikusajiliwa popote na hta kma ilisajiliwa basi baada ya tukio hili ilifutwa kwenye rekodi kwa sababu wanazojua wenyewe hivyo kila amayetaka kufanya uchunguzi wake anakwama mahali maana anashindwa pa kuanzia kuilocate meli hii ili aweze kusoma chanzo cha ajali ama vifo vya mabaharia wake.

Ingawa miaka michache baadae alitokea missionary mmoja wa kiitaliano huko visiwa vya solomon kudai alimuokota mtu aliyesalimika kwenye ajali hiyo na kwamba kabla hajaeleza chochote alifariki huko solomon islands!!!! Hivyo kama alikuwa shahidi wa muhimu basi ndio alikufa na ukweli wote wa tukio.

HITIMISHO
Baada ya kusoma kuhusu kisa hiki kutoka kwenye vyanzo mballimbali nikaona JF huwa haikosi majibu labda kuna watu wameshawahi kukutana na taarifa kuhusu tukio hili ama la kufanana na hili maana bahari ina mambo mengi basi tujuzane humu.

Hivyo swali la kutuongoza ni;
Je nini kiliwaua hawa watu na je nini kilisababisha wapigwe na mshangao/ butwaa??

Naomba kuwasilisha

ghost_ship_by_shadow_of_nemo-d8mj0xc.png
 
Sayansi ilipoishia ndipo uchawi ulipoanzia, wakienda kiroho watapata majibu ya Nini ilichokipata hiyo meli.....
kwa hiyo wazungu wameshindwa kabisa kujua ukweli wa tukio hili? kweli sayansi ina ukomo wake.Binafsi naamini viumbe vya ajabu vilihusika.
Cjui walikubwa na nn hao jamaa,kiasi wakafa kwa mshangao
 
Mkuu zitto junior Hii Story Ni Fictitious Tu!...Kwa Mtazamo Wangu!

Kwanini Nasema Hivyo?
Nitarudi Nikapata Muda Mkuu....
Nakusubir mkuu Iyegu.
zitto junior kuna muvi moja niliiona around 2013/2012 inaitwa Ghost ship(kama sijasahau) inaeleza kisa kama hiki ulichoandika watu walikua wanacheza ukumbini ukapita waya mwembamba katikati yao ukawakta vipande vipande meli zima pia kukawa na mambo ya ajabu ajabu. Sijui ndio stor yakewameitoa hapo..
Ngoja nizame kufuatilia...
 
Nakusubir mkuu Iyegu.
zitto junior kuna muvi moja niliiona around 2013/2012 inaitwa Ghost ship(kama sijasahau) inaeleza kisa kama hiki ulichoandika watu walikua wanacheza ukumbini ukapita waya mwembamba katikati yao ukawakta vipande vipande meli zima pia kukawa na mambo ya ajabu ajabu. Sijui ndio stor yakewameitoa hapo..
Ngoja nizame kufuatilia...
Duh itabidi niitafute hiyo movie mkuu i guess it's creepy...... Ila hizi story za ghost ships ni nyingi maana kuna moja huko bermuda walikuta meli ndogo ya wavuvi iko katikati ya bahari ila hakuna mtu na kila kitu kipo kwenye eneo husika ila watu tu ndio hamna duh conspirancy zikaja nyingi mno maana watu hao mpaka leo hawakuonekana
 
Kama wangekufa kwa chemical, wasingeshangaa bali wangekimbizana na kudumbukia baharini, yaani wengi wangekutwa ndani ya maji
Indeed..... Naona hapa kuna jambo kubwa zaidi lililowafanya wapigwe na butwaa hadi washindwe kukimbia maana kemikali kama unavyosema ni lazima wangekohoa huku na kule na wangevunja hata milango kujiokoa ila sio kukaa na kupigwa na mshangao hadi kifo

Kuna kitu hapa cha ajabu hapa
 
Back
Top Bottom