Kipi kifanyike ili elimu ya Tanzania iwe na tija kwa wasomi?

Kipi kifanyike ili elimu ya Tanzania iwe na tija kwa wasomi?

Jitu la Mara

Member
Joined
Feb 2, 2025
Posts
59
Reaction score
100
Machozi, majuto na kuchanganyikiwa kwa wasomi wanaomaliza vyuoni kukosa kazi mtaani. Ndoto zao kuishia kuwa simulizi ndani ya nafsi zao ni msiba mkubwa kwa Taifa letu. Ni wakati sasa wa nchi kujipanga upya. Badala ya kushusha kila mwaka kontena la wasomi wasio na pakwenda, nchi itafakari. Tuangalie nchi Kama China ambayo kwa sasa wako mbele Sana katika nyanja nyingi.

Zifuatazo ni mbinu ambazo zinaweza kufikiriwa pia;
  • Kusimamisha udahili wa kozi zote vyuo vikuu vyenye nafasi ndogo ya kuajiriwa mfano(kozi zinazotolewa CNMS pale UDOM)
  • Kushirikisha waajiri wa sekta binafsi kujua mahitaji hasa ya soko.
  • Kuimarisha VETA kimiundombinu na kutoa kozi mpya zinazoendana na Dunia ya sasa.
  • Mfumo mzima wa elimu uvurugwe Toka msingi na uanze upya kwa kuiga nchi Kama Japan na China ambapo wanafunzi Toka chekechea wanajifunza kazi za mikono na uhalisia wa maisha na sio ushindani wa nani amekuwa namba moja.
  • Serikali ihamasishe kuundwa kwa kampuni ndogondogo kwa kutoa mikopo na kuwepo kwa taasisi inayotambua na kuendeleza kazi hizo. Pia inunue kazi hizo ambazo zimekidhi ubora unaohitajika.
  • Mikopo ya asilimia 10 zinazotolewa na halmashauri za wilaya ziwe za kweli na sio dhahania au za magazetini tu.
Serikali ilete wataalamu kutoka nchi zilizzoendelea Kama China na Japan kufundisha watu kutengeneza vifaa na teknolojia mpya.
* Serikali inunue vifaa vya Kisasa kwa ajili ya mafunzo mfano tablet za wanafunzi. Mashine za hospitalini n.k


Kwa sasa niishie hapo. Karibu kwa jambo unaloona linafaa kufanyika kwa ajili ya kuinua nchi yetu kielimu na kimaendeleo.
 
1755534954249.jpeg
1755534954249.jpeg
 
Back
Top Bottom