Kipi kilitokea mpaka Pepsi ikaizidi kete Coca Cola!!

Kipi kilitokea mpaka Pepsi ikaizidi kete Coca Cola!!

Dah Cjui hata soda Mara ya mwisho nimekunywa lini... Anyway nikikumbuka nami nitachangia yupi kati Pepsi Na Coca anakimbiza....
 
Binafsi Pepsi ya chupa naipenda kuliko take away.. Coca-Cola sio mpenzi
 
Soko la Pepsi limeongezeka baada ya magereji kughundua kuwa inaondoa carbon haraka kwenye terminals za Betri za gari. Mzee , Pepsi ni janga la Afya yako. Wewe kwangua tu utumbo wako Kama terminal ya betri! Fainali uzeeni.

Kwa shida za Tz sio rhs kufikisha stage ya UZEE
 
Kwa kampuni hizi mbili brand inayoongoza kwa mauzo ni Pepsi na hii ni kutokana na ladha ya pepsi kuwa soft kutokana na aina ya upishi wanaitumia wakati ladha ya Coca ina ukakasi fulani.
Brands nyingine Pepsi inayofanya vizuri ni Mirinda fruits/nyeusi.
Brands za Coca zinazofanya vizuri ni Sprite,Krest na Fanta. Ladha ya soda hizi ni nzuri ukilinganisha na Seven up,Mirinda lemon na mirinda orange.
Kwa hiyo upishi/ladha na kingine pricing strategy wanayoifanya Pepsi umeifanya Pepsi irudishe hadhi yake kwenye soko.
 
Mimi nilikiwa mpenzi wa soda zetu zile.(coca)...ila kwa sasa napenda mirinda ya apple hatare sana...hiyo....ila kwa afya zetu...tunywe juice....
 
Kinachoibeba Pepsi ni bei bana, hili haliihitaji hata degree.

Nimeshashuhudia mara kadhaa mtu anaulizia Pepsi dukani, akiambiwa zipo Coca tu atatumia zaidi ya dakika tano kujishauri...shilingi mia ni ishu eti huku uswazi.

Ila kingine ninachokutana nacho mara nyingi ni kuwa kwenye hoteli kubwa wanalazimisha bidhaa za aina moja, yaani watakwambia hatuna bidhaa za Pepsi na mmeshakaa mezani hivyo hamna tena uchaguzi zaidi ya kuagiza kilichopo...labda wengi hao huwa wameingia makubaliano na kampuni za coca au.

Au utakuta kwenye hoteli nyingi wanakuwa na bei moja tu kwa soda zote, hapo ndio utakuta bidhaa za Coca zinatamba.
 
Wadau ili halina ubishi kwamba soda inayouza sana kwa sasa hapa nchini ni Pepsi, Kumkuta mtu anakunywa Coca ni nadra sana!
Je pepsi walifanya jitihada gani kuipiku Coca cola..je ni mbinu za kawaida kibiashara au kuna hujuma ndani yake?
Bei mkuu, pepsi wanauza 500 kwa chupa wakati coca ni 600
 
pepsi walichokifanya wamepunguza production pamoja na bei ya bidhaa yao na ndio maana demand imeongezeka na sio kwamba wamewazidi coke
 
Wadau ili halina ubishi kwamba soda inayouza sana kwa sasa hapa nchini ni Pepsi, Kumkuta mtu anakunywa Coca ni nadra sana!
Je pepsi walifanya jitihada gani kuipiku Coca cola..je ni mbinu za kawaida kibiashara au kuna hujuma ndani yake?
Cocacola walipo punguza tu ujazo na kuleta vichupa vidogo halafu bei ikabaki ile ile hapo tu ndipo pepsi alipo anzia safari yake ya matumaini na kuja kumshusha pana kazi kubwa sana.
 
hata dodoma..pepsi ndo inanyweka zaid..mpka mitaa ya vyuon
 
hata dodoma..pepsi ndo inanyweka zaid..mpka mitaa ya vyuon
 
Mnavyotutamanisha Mtasababisha mpaka twende kuzionja sasa
 
Soko la Pepsi limeongezeka baada ya magereji kughundua kuwa inaondoa carbon haraka kwenye terminals za Betri za gari. Mzee , Pepsi ni janga la Afya yako. Wewe kwangua tu utumbo wako Kama terminal ya betri! Fainali uzeeni.

Kwani matumbo yetu yameundwa na carbon kwamba yatakuwa eroded??? Au hujui binadamu tumboni tunazalisha strong acid same as battery acid ambayo tone moja tu linatoboa kipande cha mti ndani ya dakika tu.

Issue ni kuwa matumbo yetu yameumbwa pamoja na epithelial cells ambazo zinaproduce mucus and bicarbonate solutions ambazo ndio zinalinda matumbo yetu.
So kama wewe ni mnywaji wa pepsi we kunywa tu kuna vitu vitakusaidia kukulindia tumbo lako lisigeuzwe terminal za batteries. Ila tu kwenye kuongezeka uzito hakuna guarantee.
 
Wadau ili halina ubishi kwamba soda inayouza sana kwa sasa hapa nchini ni Pepsi, Kumkuta mtu anakunywa Coca ni nadra sana!
Je pepsi walifanya jitihada gani kuipiku Coca cola..je ni mbinu za kawaida kibiashara au kuna hujuma ndani yake?
Labda dar, sio mikoani
 
Inaonekana unaishi dar tu hujasafiri mikoani we we,,,kuna sehem unaweza tafuta soda ya pepsi wauzaji wakakushangaaa,,,hivyo hvyo kama vocha ya Tgo... Tembea uone
 
Back
Top Bottom