Kipi kimemsibu Koke wa Atletico Madrid?

Kipi kimemsibu Koke wa Atletico Madrid?

Mchochezi

JF-Expert Member
Joined
Feb 29, 2012
Posts
10,962
Reaction score
7,830
14413677795_446bf24c6e.jpg

Kuna kipindi alitajwa kama mrithi wa Xavi Hernandez kwa umahiri wake wa kutandaza soka hasa katika nafasi ya kiungo mshambuliaji na kuzua gumzo kwa timu mbalimbali kutaka kumsajili, lakini kwasasa inaonekana kama nyota yake imeanza kufifia na hakuna timu yoyote inayomtaka tena na wala hasikiki tena na zile pasi zake murua bila kusahau assist. Je Koke ameisha kiwango katika umri wa miaka 25 tu au ni nini kingine kimemsibu kiungo huyu matata?
 
Alikuwa fomu sana msimu ambao Atletico alifungwa fainali ya Uefa na Real Madrid. Tokea hapo amekuwa hapati nafasi hata kwenye kikosi cha timu ya Taifa.

Kuna kipindi Chelsea walimtaka kwa udi na uvumba wakaambulia patupu. Nasikitika kuona kipaji cha hali ya juu cha Koke kikiwa kinafifia.
 
Koke muda si mrefu aliongeza mkataba na Atleti mpaka 2024. Kama unaelewa soka, hicho ndicho kimemsibu.
 
Koke bado yupo vizuri ndio maana national team anaanza mwanzo mwisho

Wakati Barca wanantaka alisaini miaka 5 au 6 na kusema haondoki ATM ,labda husikii tetesi zake ukadhani kaisha la hasha alishatamka wazi ATM haondoki na katia saini miaka 6

Subiri mechi za timu za taifa zianze lazima aanze

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Koke??? namkubali mno mpaka kesho..
Ndie uti wa mgongo wa ATM...
 
Huyu jamaa ni mgumu mi namkubali kishenzi asee ni undava tu uwanjaani

huwezi jua
 
Alikuwa fomu sana msimu ambao Atletico alifungwa fainali ya Uefa na Real Madrid. Tokea hapo amekuwa hapati nafasi hata kwenye kikosi cha timu ya Taifa.

Kuna kipindi Chelsea walimtaka kwa udi na uvumba wakaambulia patupu. Nasikitika kuona kipaji cha hali ya juu cha Koke kikiwa kinafifia.
Lugha gongana
Koke bado yupo vizuri ndio maana national team anaanza mwanzo mwisho

Wakati Barca wanantaka alisaini miaka 5 au 6 na kusema haondoki ATM ,labda husikii tetesi zake ukadhani kaisha la hasha alishatamka wazi ATM haondoki na katia saini miaka 6

Subiri mechi za timu za taifa zianze lazima aanze

Sent using Jamii Forums mobile app

Pogba wa tz nchi imekushinda!
 
Kuna kipindi alitajwa kama mrithi wa Xavi Hernandez kwa umahiri wake wa kutandaza soka hasa katika nafasi ya kiungo mshambuliaji na kuzua gumzo kwa timu mbalimbali kutaka kumsajili, lakini kwasasa inaonekana kama nyota yake imeanza kufifia na hakuna timu yoyote inayomtaka tena na wala hasikiki tena na zile pasi zake murua bila kusahau assist. Je Koke ameisha kiwango katika umri wa miaka 25 tu au ni nini kingine kimemsibu kiungo huyu matata?
Badala ya koke labda ungeuliza Nini kimemsibu Ustaadh Arda Turan!

Pogba wa tz nchi imekushinda!
 
Mleta mada inaonesha la liga hauitazami mara kwa mara. Koke kajifunga ATM. Koke ni Mchezaji mzuri ila ukisema la liga lazima utaongelea wachezaji wa barca na Real. Ila ukikutana na mtu ambaye si shabiki ila ni mpenzi wa ligi atakwambia timu iliyotoa burudani nzuri la liga msimu uliopita ni CD EIBAR.
 
Back
Top Bottom