Kipi kimemsibu Koke wa Atletico Madrid?

Kipi kimemsibu Koke wa Atletico Madrid?

tatizo mechi za atletico mnaangalia kwenye uefa tu hamwezi kuona kazi aliofanya koke msimu uliopita. husiki tim zikimtaka kwasababu amesaini mkataba mpya mwaka huu pia huyu jamaa ni atletico madrid damu yaani ameanza soka kwenye academy yao tangia utotoni ni shabiki wa atletico.....real Madrid na barca wanalijua hili ndo mana wamekataa tamaa za kumsajili.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Koke wakaida sana sema aliibuka tu now karudi kwenye uwezo wake viungo bwana enzi hizo gaizka mendieta roman riqueme pavel nedved edgar davids andrea pirlo claude makelele sahv wachezaji wa kawaida sana
 
Koke wakaida sana sema aliibuka tu now karudi kwenye uwezo wake viungo bwana enzi hizo gaizka mendieta roman riqueme pavel nedved edgar davids andrea pirlo claude makelele sahv wachezaji wa kawaida sana
kila nabii na zama zake
 
JORGE RESURECCIÓN a.k.a KOKE

....Wengi wetu tumejizoesha na tukazoea sana kuhukumu watu na matukio yao katika umbo la nje..
Wengi tunapomtazama Jet Lee katika Movies zake tunaiona China ndani yake,,Tunapomtazama Bruce Lee tunaiona China ndani yake..
Lakini kiuhalisia China imekuwa China kwa sababu ya wapiga kazi kupita kiasi wa kichina.


Katika jiji la Madrid kuna timu kuu mbili ambazo ndizo habari ya jiji la Madrid..Real Madrid(Los Blancos) na Club Atletíco de Madrid(Los Rojiblancos)..
Pale Atletíco madrid kuna Mtu anaitwa Diego Pablo Simeone..
Jamaa ameifanya Atletí kuwa moja ya timu ngumu na zenye ushindani mkubwa sana barani europa..
Jamaa kawabadilisha wachezaji wengi wa kawaida kuwa watu wagumu..watafuta mafanikio katika hali zote..


Amekwishashinda ubingwa wa ligi kuu Hispania(La liga),Copa del rey,lakini pia kufika fainali mbili za uefa champions league bahati hakufanikiwa kuchukua hata ndoo moja.
Katika vurugu zote za Simeone ulaya kuna wachezaji ambao wametajwa sana midomoni mwa mashabiki wa Estadio Vicente Calderon na nje ya Calderon..Wachezaji kama Diego Costa,Diego Godin,Joao Miranda,Thibaut Curtois,Felipe Luiz,Antoine Griezmann,Yannick Ferreira Carrasco wametajwa mno katika mafanikio ya Simeone na Atletico yake..


Nyuma ya kundi lote hili wa watu wa shughuli kubwa kubwa(BIG OCCASIONS) kuna jembe moja ambalo ndo kama Choir Master katika show zote..Huyu jamaa sio mwingine bali ni Jorge Resureccion wengi wetu tumamzoea kama KOKE mzaliwa wa kitongoji fulani kinaitwa Vallecas miaka 25 iliyopita..Mnamo January 8,1992..
Koke ni moja ya wachezaji waliozaliwa eneo timu ilipo wakaanza kuichezea tangu hatua zote za soka la watoto mpaka kuingia moja kwa moja katika timu ya wakubwa..Kwani Alianza soka lake katika academy za Atletico de Madrid akiwa na miaka 8..akakomaa mpaka kuingia haraka kikosi cha under 15 hatimaye ngazi za Vijana za Timu ya Taifa U-1,U-17,U19,U-20 hata ile U21 ambao walichukua ubingwa wa Mataifa ya ulaya mwaka 2013..Naye akiwemo katika kikosi bora cha mashindano(Tournaments Dream Team)..



Koke amekuwa nguzo muhimu kwa Atletico de madrid kwani ndiye kiungo pekee pale atleti ambaye anaweza kucheza nafasi yoyote ya kiungo..iwe kushoto,kulia,au kati na wakati fulani Fundi wa Mpira Xavi Hernandez Creus aliwahi kukaririwa akisema,"Koke ni moja kati ya viungo wanaoweza kusimama kwenye nafasi yangu ya kiungo wa kati vizuri zaidi kwa zaidi ya miaka 10"..
"Ni kiungo mwenye ubunifu(creativity),Ufanisi wa miguu yote(tremendously efficient on both feet) na umakini katika kazi zake uwanjani"Alikaririwa Xaví ambaye ni gwiji la sehemu kiungo katika taifa lenye utajiri mkubwa wa viungo wa soka..



Koke akiwa amezungukwa na Mkongwe Gabriel Fernandez(Gabi),Thiago Mendes,Thomas Partey,Juanfran,Felipe Luiz,Saul Niguez,Adrian Lopez na Raul Garcia tangu 2013 amekuwa mtu hatari sana Atlerico de madrid..
Anakaba,,anapiga pasi za karibu,za mbali na za mwisho(killer passes) amekuwa mtu wa kuamua matokeo katika mechi nyingi sana ..Moja inayokumbukwa ni ile mechi ya kuamua(decisive game) nani awe bingwa wa La Liga msimu wa 2013/2014 ambazo goli lake liliwapa nafasi kya kupata draw mbele ya Barcelona na kutawazwa kuwa mabingwa wa La Liga baada ya miaka mingi sana..


UKIKUTANA NA ATLETICO DE MADRID ama Los Colchoneros Basi usihangaike sana na Antoinne Griezmann,Carrasco, Angel Correa,Saul Niguez n.k
Wewe mkatie umeme Koke Resureción..basi utakuwa umemvuruga akili Diego Pablo Simeone..
Wekeza Muda wako sana katika game za Atletico kumtazama Koke na Movement zake Ndipo tutaongea lugha inayofanana..

[HASHTAG]#footballaddicted[/HASHTAG]
 
Hongera mleta uzi at least umefanya la maana sio kila siku watu ni messi vs ronaldo huku wanasahau vipaji kama hivi

Kiukweli huyu jamaa ukimuweka katikati na saul niguez pamoja na wagumu kma Augusto fernandez na Gabi inaeleza kwanni imefungwa magoli machache zaidi ulaya nzima kwa miaka kadhaa mfululizo maana jamaa wanakaba haswaaaa

Nachopendea atletico hawana kikosi cha masuperstar ila wanajituma sana kana kwamba kila mechi ni fainali.... Credit to Diego simeone
 
Hongera mleta uzi at least umefanya la maana sio kila siku watu ni messi vs ronaldo huku wanasahau vipaji kama hivi

Kiukweli huyu jamaa ukimuweka katikati na saul niguez pamoja na wagumu kma Augusto fernandez na Gabi inaeleza kwanni imefungwa magoli machache zaidi ulaya nzima kwa miaka kadhaa mfululizo maana jamaa wanakaba haswaaaa

Nachopendea atletico hawana kikosi cha masuperstar ila wanajituma sana kana kwamba kila mechi ni fainali.... Credit to Diego simeone
Upendo mmoja ndugu

Kama ID yako inasadifu ni ww kweli basi ghafla ninakukumbuka unahahaa na Liverpool yenu...

Naona Salah naye yupo kwa muda kabla hajaamua kwenda vilabu vyenye maziwa na asali (kubeba trophies)[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Tanzania yetu majungu Na unafiki ndio twaweza kuchukua kombe. Soccer tuwaachie Brazil Na Argentina
 
huyu mwanadamu muda wote yupo kikazi zaidi
hi-res-66f1629456cba2a17cb4d91dc617bc42_crop_north.jpg
 
Nitaanza kumfuatilia katika mechi zake.
Mechi za A.Madrid ninapomkosa Torres huishiwa moody.
Jana (13/01) nimeacha goal moja bila nikaenda kulala.
 
Back
Top Bottom