Kipi kinakatika umeme au waya

Je, maji yanapoacha kutoka kwenye bomba bila kulifunga, je itakuwa bomba limekatika au maji? Maana kubwa hapa ni ile 'flow' au 'current'.
 
Vyovyote utakavyotamka au kutumia neno lakini maanake ni nchi kuwa gizani kwa sababu context iko wazi. Unafikiri neno likikosewa wakati kwa situation iliopo ujumbe ni clear Jairo, Ngeleja, Malima na JK wata-escape punishment kutoka kwa wananchi?
.....................nalo pia jibu..........naendelea kusubiria wataalam
 
Kiswahili fasaha ni umeme-UNAZIMIKA,na waya UNAKATIKA.
 


Maana ya maneno hutegemeana na jinsi neno lenyewe linavyotumika katika sentensi. Kwa mfano neno Kukatika linatumika zaidi kwenye kuelezea kitu au hali ambayo ina mwanzo A na ina mwisho B katika unyoofu (linear). Kwa mfano tutasema, kamba imekatika, waya umekatika, nguzo ya umeme imekatika. Lakini pia kukatika na kuvunjika kunaweza kutumika kwa kubadilishana. Mfano tunaweza kusema, mkono au mguu umevunjika/umekatika.

Neno kuvunjika zaidi linatumika katika kuelezea hali au kitu kilichosambalatishwa na kisichokuwa na umbo nyoofu bali chenye umbo bapa. Kwa mfano. Tutasema, kioo cha gari kimevunjwa au kimevunjika. Glasi ya maji imevunjika/imepasuka, nyumba imevunjwa/imebomolewa.

Kwa hiyo utaona kwamba matumizi yanategemea hali na mazingira.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…