Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
.....................nalo pia jibu..........naendelea kusubiria wataalamVyovyote utakavyotamka au kutumia neno lakini maanake ni nchi kuwa gizani kwa sababu context iko wazi. Unafikiri neno likikosewa wakati kwa situation iliopo ujumbe ni clear Jairo, Ngeleja, Malima na JK wata-escape punishment kutoka kwa wananchi?
mkuu wangu rungu, asante kwa kushukuru...
sasa tuendelee na mada...tofauti ya kukatika na kuvunjika!
kukatika...kwa mazoea(sijui kwenye kamusi wanasemaje, hapa natumia uzoefu tu) tunatumia neno hili katika vitu visivyo na maumbile yenye kuonekana kama huduma mbalimbali mfano huduma ya umeme imekatwa, huduma ya maji imekatwa, huduma ya simu imekatwa. na neno mbadala kwa baadhi ya huduma ni kusitisha..mfano kuduma ya kusajili namba za simu imesitishwa kuanzia tarehe fulani mpaka tarehe fulani. tanbihi; kwa makosa watu hutumia neno imesimamishwa badili ya imesitishwa.
Kuvunjika...kwa mazoea tunatumia neno hili kwa vitu vyenye maumbile yenye kuonekana na ambavyo ends mbili zinapokosa kuungana kwa kutenganishwa na ikiwa katika tendo la kutenganisha kuna sauti inazalishwa. ni kwa mantiki hiyo njiti ya kiberiti inavunjika na waya unakatika(kumbuka waya unapokatika huwa hakuna sauti yenye kusikika kwa uwazi.
lakini kama alivyosema mkuu Rungu hapo juu...hii mada ni ngumu pengine wakija wataalamu humu wataweza kutusaidia...bahati mbaya mzee wetu wa mbinu za kiswahili katika TBC1, Suleiman Hegga, sidhani kama anapita maeneo haya.