Kipi kinakupa furaha ukiwa Jamiiforums?

Kipi kinakupa furaha ukiwa Jamiiforums?

Idn

New Member
Joined
Sep 28, 2021
Posts
3
Reaction score
1
Moja wapo ya eneo katika utandawazi linalo kuwa kwa kasi sana hapa nchini basi ni utandawazi wa teknolojia ya simu, na moja wapo ya simu zinazoenea na zenye soko sana hasa maeneo ya mijini ni smart phone(jina maarufu simu janja) na pia ukweli huu haupingiki moja wapo ya jamii ya watu wanao tumia sana simu hizi ni vijana, wakiongozwa na wale waliopo vyuoni.

Tatizo sio simu wala ukuaji wa hii teknolojia ya simu, bali tatizo ni namna mtu anavyotumia hii fursa ya ukuaji wa teknolojia ya simu.

Kila kitu ni kizuri ila kuna matumizi mabaya katika kila kitu kizuri.

Siku moja nilimuuliza rafiki yangu mmoja maswali haya 3.

1. Je ni kipi kinampa furaha?
akanijibu "kuwa online mitandaoni, nikiwa na uwezo wa kuingia instagram, whatsapp, facebook au youtube, hapo mimi hufurahi!"

2. Nikamuuliza kuna biashara unaifanya kupitia mitandao ya kijamii.?
Alijibu "hapana"

3. Vitu gani unapenda kuangalia au kusikiliza?
Alijibu "vichekesho na habari za watu mbalimbali maarufu"

Fikiri huyu ndugu siku amekosa bando, kwanza hata kuwa na furaha, na je anatumiaje bando lake?

Tulinde fikra zetu na tutumie vizuri hii fursa, kwani kuna mazuri na mabaya mitandaoni, kuna watu wanafanya biashara, ujasiriamali na wengine watakuwa washindi kupitia shindano la andiko chini ya JAMII FORUMS.

Hufanyi biashara, elimika kifikra, zipo asasi na watu binafsi ambao wanaelimisha kupitia mitandao ya kijamii.

JAMII FORUMS ni miongoni mwa asasi mbayo inafanya hivyo.
Kila kitu ni kizuri ila kuna matumizi mabaya katika kitu kizuri.

Tue_28_09_2021_21_39_11.png
 
JF kwa asilimia kubwa imefanya nitumie bando kwa manufaa na sio kushinda kufuatilia maisha ya watu wasio niongezea chochote na upuuzi mwengine#IdumuJF
 
  • Thanks
Reactions: Idn
Asante sana, ila ni wachache wanaotumia vizuri bando lao.
 
Nainjoi sana kupigwa Ban humu yaani hadi raha ukiona Avatar inasoma BANNED
 
Mi nainjoi likes na quotes inanihakikishia watu wamesoma bandiko langu.
 
Back
Top Bottom