Kwangu mimi maumivu makali niliyopitia
Kufiwa na mamangu mzazi mwaka wa 3 ila kila nikikumbuka natokwa na chozi....yote tisa hakuna kitu kibaya kama kuona mtu wako unaempenda lazima afe una ujua haya magonjwa .tu akiumwa sana mnakuwa mnajua haponi
Maumivu ya pili mpenzi wangu niliyekaaa nae miaka sita ...mmmh huyu alivyoondoka sikumia mwanzoni ila roho iliniuma hapo kipato kimeyumba mwanamke kasepa wewe maumivu pasi inasubiri....
Maumivu mengine niliwahi pitia ni kusoma na watoto wa matajir wakati wewe ni mtoto wa masikini wenzio wanatumiwa pocket money laki moja wewe mama ako anakutumia 15000tsh ....utakula ugali wa shule hadi ufe
Basi nashukuru mungu baada kumaliza shule nilipata kipato kizuri sana na maisha yanaenda biashara za china zinasadia huwa nasahau maumivu
La mwisho siku narudi nyumbani kwangu saa tatu usiku nakaa sebuleni nashangaa mchumba wangu anatoka chumbani anasema magufuli kafariki sito sahau naangalia kwenye simu nakuta kila kapost niliumia sana ile siku........ kama kafa ndugu yangu wa karibu hadi leo nikionaga picha ya magu nasemaga mungu