Kipi kinavuja?

Kipi kinavuja?

Chomsky

Member
Joined
Jul 15, 2012
Posts
31
Reaction score
5
Upi ni msemo sahihi wa Kiswahili sanifu kati ya misemo ifuatayo?

a. Ndoo inavuja

au

b. Maji yanavuja?

Tusaidiane katika hili wadau wa Kiswahili.
 
ndoo inavuja ni sahihi kabisa,maji yatavujaje mkuu
 
Mtafute mwalimu Masebo wa Mkwawa ama Kalembo wa Dakawa enzi hizo ndo walikuwa walimu wa Kiswahili Tanzania nzima hakuna aliekuwa anawafikia. Nasema hivo maana wengine watakuyeyusha tu
 
ndoo inavuja(maji ni kioevu kinachowekwa kwenye ndoo.Hakiwezi kuvuja.bali chombo kilchobeba kioevu hicho chaweza kukivuja)
 
Back
Top Bottom