Mhe. Waziri Mkuu aliwatuma Mawaziri wa kisekta kubaini mpaka halali wa Hifadhi ya Serengeti na Wilaya ya Tarime maeneo ya Gorong'a na Gibaso baada ya kilio cha muda mrefu kutoka kwa wananchi kuhusu mpaka huu.
Matokeo ya Tume hiyo ni kuwa malalamiko ya wananchi wa eneo husika hayana mashiko. Sasa ninakuja na swali: GN ya alama za mpaka huu uliwekwa katika miaka 1958 wakati Watanzania kwa wakati huo Idadi ya Watanzania wote ni kama 8 millioni. Mpaka sasa imepita takriban miaka 65 tangu alama hizo kuwekwa na kwa sasa idadi ya Watanzania inakadiriwa kufikia 61 millioni.
Inawezekana kwa wakati huo idadi ya wananchi kwa maeneo yanayogombaniwa walikuwa watu 200 na sasa inawezekana wako 30000. Kama Serikali ni serikali inayojali wananchi na ni Serikali sikivu je wanyama ni bora kuliko wananchi?
Kama wananchi wameongezeka kwa nini Serikali isisogeze alama za GN kilomita 50 ndani ili wananchi wapate nafasi ya makazi?
Ninaishauri Serikali kwa kuwa watu wameongezeka sana na thamani ya binadamu haiwezi kulinganishwa na mnyama basi ni vema Serikali ifikirie kusogeza GN ndani ya kilomita 50 ili mgogoro huu uweze kuisha jumla.