Kipi ni chuo bora hapa Tanzania?

Vyuo Vyote uozo..kazi kutengeneza mafisadi.
 
Kila mtu anasifia ubora wa chuo chake na si akili na ujuzi wake,hasa madenti wa udsm wanajikweza kua ndo no
 
ndiyo maana mkatoa rais legelege Jk

mbona umeangalia wabaya tu, wabora hamuwaangalii?

Beside, kwani JK kwa upande mwengine hajafanya ya maana? Unataka kuniambia hajafanya lolote toka ahitimu? Usiwe na upendeleo ukinijibu.

Tabia nyingine ni za mtu mwenyewe na sio chuo alichosoma.
 
Kila mtu anasifia ubora wa chuo chake na si akili na ujuzi wake,hasa madenti wa udsm wanajikweza kua ndo no

hatujisifu...kama unaona tunajisifia na wewe sifia chako basi!
 
kwamtazamo wangu chuo bora hapa bongo hakuna.Chuo ambacho kinaweza kuwa bora angalau ni mzumbe, nasema hayo kwa kuangalia mashindano ya Zain Africa challenge Universities .Mzumbe angalau kilifurukuta, lakini udsm ni viroboto tu. habari ndi hiyo.
 
acha kuchangia mada kwa kutoa hoja mbovu hivyo kama una njaa fanya ule kwanza maana akili yako iko mbali kabisa,huwezi kukihukumu chuo kwa kuangalia wajinga wajinga wachache tu walioshiriki hiyo michuano,Majembe hawana habari na hizo takataka...
 
IFM kina sifa ya chuo cha kata! kinachukua wanafunzi vilaza.
ndugu nenda kaangalie kwenye records za say CPA mbona IFM inafanya vizuri sana kuliko UDSM hao maprofessor wamewasaidiaje wanafunzi mbona wanaonekana vilaza kwenye proffesional studies?
 
mi nadhani ungelinganisha college zinazotoa fani zinazofanana mfano: ST.JOSEPH,CoET,MIST na DIT kwa maswala ya Engineering
na kwa CBE ULINGANISHE NA SHULE YA BIASHARA UD,NA KWENGINEKO NDO UTAPATA JIBU.
 
acha kuchangia mada kwa kutoa hoja mbovu hivyo kama una njaa fanya ule kwanza maana akili yako iko mbali kabisa,huwezi kukihukumu chuo kwa kuangalia wajinga wajinga wachache tu walioshiriki hiyo michuano,Majembe hawana habari na hizo takataka...

sasa kama wenye akili walikuwepo na hawakwenda kutetea ubora wa chuo chao sisi tutapima vipi ubora wa hicho chuo unachokisifia.mimi naona mkubali tu,ud limebaki jina tu,lakini kuhusu ubora wa taaluma,wanaohitimu hapo wanaishia na chawa kichwani.
 
kama UD imebaki jina tu unamaana hao waliotoa rank ya dunia ni wajinga? Unafikiri walitumia vigezo gani?

Mimi zamani nilikuwa naamini Udsm ni jina tu, ila baada ya kuja hapa Udsm nimeona nilikuwa ninaamini ujinga tu. Udsm kuna sectors inajitahidi sana.
 
its beter to conduct Reasearch before making conclusion which is better,sort out criterior then make measurement,i m sure jibu litapatikana tu.
 
Swali rahisi sana hilo, UDSM ndio chuo bora kwa Tanzania, sio kwamba nakisifia, hapana....ndio ukweli huo.
HABARI NDIO HIYO! KAMA UNABISHA ANDAMANA.

Soon kitazidiwa na vyuo vya kata,me naona kwa sasa kinapoteza mwelekeo kinataka kuwa chuo cha siasa.
 
Wasomwaji wa siku hizi bwana,ndo wale wale eti darasa la saba na form four hawana akili.Angalau hopo kale sisi wa darasa la saba tulikuwa tunatambuliwa na kutoa mchango mkubwa kwenye jamii siyo hawa elimu makaratasi,makabrasha,.najiuliza mtu kama BUJIMA akienda mtaani kwao inakuwaje si taaabu kweli kweli.
 
ndugu nenda kaangalie kwenye records za say CPA mbona IFM inafanya vizuri sana kuliko UDSM hao maprofessor wamewasaidiaje wanafunzi mbona wanaonekana vilaza kwenye proffesional studies?

Kama matokeo ya CPA ndio fact yako, basi UDSM kitabaki kuwa bora. Ongea kwa fact, sio kwa maneno unayosikia. Nenda website ya NBAA, kwenye news fungua Institution Examination Performance - Module E & F for the past three examination sessions (May 2010 to May 2011).

UD ndio chuo kinachofaulisha wanafunzi wengi zaidi wa CPA kuliko chuo chochote Tanzania. 33% ya wanachuo wa UD waliokaa kufanya mitihani ndani ya hiko kipindi wamepata CPA, wakati IFM ni 20.5% tu.

Go to read then come back to speak!
 
karibu.
 
Dah kweli "mwamba ngoma huvutia kwake",chuo tulichosoma sisi siwezi kusema ni bora au la ila utafiti ni sehemu ya maisha hapo chuoni, huwezi zua mjadala bila base yenye maana,thread iko broad sana coz ubora unaoongelewa unazingatia base au msingi gani?
*# of lecturers?
*uzuri wa majengo?
*performance katika ajira?
*publication and research?nk aliyeanzisha thread katuacha hewani, katika kupima vitu viwili viwepo vigezo,defend yourself ukisema X is better than Y tupe sababu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…