Kipi ni chuo bora kwa kozi za Engineering kati ya UDSM,DIT na MUST ?

Kipi ni chuo bora kwa kozi za Engineering kati ya UDSM,DIT na MUST ?

kama lengo lako ni kuwa mhandisi ulieiva nakushauri nenda udsm..pia kama lengo lako ni kuwa fundi mchundo uliyeiva nenda DIT.
asante

waropokaji buana sijui mna nini lakini....hao DIT unaowaita fundi mchundo ndio syllabus yao inatumiwa na udsm....yaani kwa ufupi ni kiwa udsm walicopy mzigo kutoka dit
 
waropokaji buana sijui mna nini lakini....hao DIT unaowaita fundi mchundo ndio syllabus yao inatumiwa na udsm....yaani kwa ufupi ni kiwa udsm walicopy mzigo kutoka dit
Unajua COET vizuri hile ilikuwa inatwa FOE imeazishwa mwaka 1973 kipindi hicho hiyo hicho chuo za mafundi mchundo DIT( DTC) takataka
 
Hivi kati ya vyuo tajwa hapo juu kipi kinanoa vizuri wanafunzi kinadharia na vitendo katika kozi za engineering?,hasa Electrical engineering.
Kama akili ziko za kutosha Nenda DIT
DIT kwenye electrical Engineering ya vitendo ni moto wa kuotea mbali
 
DIT ilikuwa zamani lakini siyo kwa sasa hivi .Maana wakati huo hiki chuo kilikuwa kimeanzishwa mahsusi kwa wale graduates ambao walianzia elimu ya ufundi kuanzia technical sekondari na walikuwa wanachuja kwelikweli kujiunga walikuwa wanachukua wale vipanga wa namba.
Kiuhalisia udsm (COET) itabakia kuwa udsm nembo ya taifa bado wanatunza ubora wa elimu.DIT siku hizi hata ukiwa na pass za kawaida unachukuliwa na cheti wanachukua.
Kama umefaulu vizuri form six unataka kusoma Engineering best university ni UDSM ukiwa bado kijana bado udsm inamaintain standard.Ila ukiwa kijana ukienda vyuo vingine kama DIT utakutana na wazee wanasoma program zao wanaziita evening program watakuchanganya wakunyime uwezo wa kujitegemea kufikiria na kusoma kwa bidii nafikiri umenielewa.
Mkuu unabisha nini? Au mpaka uambiwe wengine tumeshawahi kufundisha huko ndiyo uelewe?
 
Kama umefaulu vizuri na umechaguliwa nenda UDSM kwa Engineering .DIT ilikuwa zamani kabla hawajaanza kuchanganyachanganya mara evening program mara full time.UDSM bado wanamaintain standard huwezi kusoma udsm kama ufaulu wako wa form six haueleweki eleweki.Halafu ukiwa kijana kasome na vijana wenzako huko udsm ukisoma na hao wazee wa DIT watakuchanganya utakuwa unapiga nyanga zako unaona wazee wanakula bata mwisho wa siku wanachukua degree na zingine GPA kubwa kuliko wewe kijana unayekesha nafikiri umenielewa
Unafikiri DIT wana degree za kuhonga kama huko unapopanadi? Hatutaki kuandika mengi, sisi tunafahamu mengi. Mwisho wa siku isije ikaonekana tuhuma au unachafua jina la Chuo fulani.

DIT kuzungusha ni rahisi sana ukiwa unasoma kama usomaji wa UDSM.
 
Uzuri wa DIT ya siku hizi hata ukiwa mzee ambaye ulishajichokea mpaka akili imechoka na huna pass za kukuwezesha kusoma UDSM ukiingia DIT unasoma engineering evening program bata unakula na mwaka wa mwisho unachukua degree yako GPA ya kutosha wale vijana full time wanakata nyanga wanabaki kushangaa.Habari ndiyo hiyo mjini shule
Unaongopa kwa faida ya nani? Mbona Udsm evening program zipo? Point yako hasa ni nini?

Ila fahamu kuwa bila engineer wa DIT hata hii Jf usingeijua.
 
Kiufupi vyuo vyote(DIT & COET) ni vizuri uzuri wa mtu hauangalii chuo alichosoma ila ni juhudi yake na bidii katika masomo na kujituma akiwa kazini hizi zingine hapa ni mbwembwe na ushabiki tu.Maana ukienda kazini unakuwa na General knowledge ya Engineering sasa kujituma kwako kule kazini na utundu kutaka kujifunza vitu vingi ndiyo mafanikio yako.
Unaongopa kwa faida ya nani? Mbona Udsm evening program zipo? Point yako hasa ni nini?

Ila fahamu kuwa bila engineer wa DIT hata hii Jf usingeijua.
Zu
 
Unafikiri DIT wana degree za kuhonga kama huko unapopanadi? Hatutaki kuandika mengi, sisi tunafahamu mengi. Mwisho wa siku isije ikaonekana tuhuma au unachafua jina la Chuo fulani.

DIT kuzungusha ni rahisi sana ukiwa unasoma kama usomaji wa UDSM.
Kuna mwenzako kutoka chuo chako unachosema hakitoi degree za kuhonga alikuwa haoni tofauti ya graduates wa bachelor degree ya electronics na fundi mhitimu wa darasa la saba. Sasa kama tu alumni anashindwa kuona utofauti wake yeye na std 7 utatuaminisha vipi kwamba degree ya DIT ni bora kuliko ya UDSM?
 
Back
Top Bottom