mkemia mkuu mstaafu
Member
- Nov 21, 2017
- 51
- 143
Mkuu, wewe ni lulu kwenye hii forum✓ Msimu wa kupandwa
Dengu huwa inalimwa kipindi Cha mwisho cha mvua Yan ikabaki week moja mvua kuisha mfano singida wanalima kuanzia mwezi wa 4 mwishoni hadi 6 mwanzoni
Alizeti huwa inalimwa baada ya mvua za kwanza kuisha maana ikilimwa mwanzoni huwa inakuwa vigumu kuvuna kutokana na mvua kuwa kubwa mfano singida inalimwa mwezi wa 1 katikati hadi wa pili mwishoni
✓ Palizi
Dengu huwa aifanyiwi pilizi maana inapandwa miezi ya mwisho baada ya mvua kuanza kuisha
Alizeti inataka palizi moja au mbili inategemeana na nyasi
✓ Ndege
Dengu huwa aishambuliwi na Ndege yoyote yule Wala panya
Alizeti huwa unaliwa na Ndege kuanzia siku ya kupanda hadi kuvuna ivyo itakulazimu kuhamia Ndege Yani kufukuza
✓ Masoko
Dengu huwa inaitajika kwa wingi gunia huwa linauzwa 140000 kipindi Cha kuvuna inaweza kupanda hadi kufika 230000
Alizeti huwa inaitajika kwa wingi gunia huwa linauzwa 35000 kipindi Cha kuvuna inaweza kupanda hadi 100000 inategemeana na majira
✓ Utunzaji
Dengu iana gharama sana kwenye kutunzaa maana aishambuliwi na wadudu lkn inabid iwekwe kwenye sehemu kavu ili isipate ukungu
Alizeti inabid itunzwe sehemu ambayo panya awezi kuingia maana ni hatari sana anaweze kula kiasi kikubwa endapo wakiwa wengi
✓ Maandalizi Baada ya kuvuna
Dengu ni vigumu kuibangua kwenye maganda yake ivyo utaitaji vibarua wa kutosha au utumei tractor ili kupata zile punje zake
Alizeti sio vigumu sana kuitoa kwenye kichwa chake ivyo vibarua wachache wataitajika
✓ Kuongeza thamani
Dengu endapo iki kobolewa huwa inauzwa 3000 kwa kilo lkn isipo kobolewa inauzwa 1500 pia mashine za kukoboa huwa ni chache sana ivyo wakulima wengi wanauza 1500 kwa kilo
Alizeti endapo ikikamuliwa mafuta huwa nayaunzwa 4000-7000 Kwa liter pia mashudu Yana unzwa 300-700 kwa kilo
✓ Upatikanaji wa Mbegu
Dengu upatikanaji wa Mbegu ni mgumu sana ivyo wakulima wengi huwa wanaludia mbegu zile zile kila mwaka ivyo upelekea mavuno kuwa chini
Alizeti upatikanaji wa Mbegu ni lahisi sana maana Kuna mbegu za kisasa na kienyeji ivyo mkulima ana uwanja ukubwa wa kuchagua mbegu ipi ya kulima
✓ Udongo
Dengu huwa inalimwa kwenye Udongo mweusi Yani tindiga wengine wanasema mbugani maana inatunza unyevu wa kutosha
Alizeti inaweza kulimwa kwenye Udongo wowote ule lkn chachu ya Udongo isizidi 6.5-8.5, pia usiwe unatwamisha maji
✓Matumizi ya mbolea
Dengu huwa aiwekewi mbolea maana ni jamii ya mikunde ivyo inaweza kufanya nitrogen fixation lkn unaweza kutumia mbolea za maji zenye kuwango kibuwa Cha phosphorus
Alizeti huwa inaitaji mbolea kwa ajili ya ukuaji na kuzaa ivyo mkulima inabid uweke mbolea mala moja au zaid itategemeana na Shamba lako
✓ Kiasi Cha mbengu kwa hekari moja
Dengu inahitaji kilo 15 za mbegu ili uweze kupanda kwenye eneo la hekari moja maana huwa inamwagwa ivyo inaitajika kwa kiwango kikubwa
Alizeti inahitaji kilo 2 za mbegu ili uweze kupanda kwenye eneo la hekari moja maana huwa inatumia spacing ya 60 cm × 30 cm
Sijui ni nini umekiacha hapa aisee.
Bravo.