Kipi ni kiwango sahihi cha pombe kali kiafya?

Gloriamagret

Member
Joined
Jun 12, 2023
Posts
47
Reaction score
155
Mimi nakunywa konyagi ndogo 250 mls kwa siku, tena nakunywa na maji lita moja kwa pamoja.

Nakunywa kidogo kidogo kwa masaa matatu kutoka saa moja usiku mpaka saa nne usiku, nachangamka kidogo, naingia home naoga, nakula na kulala safi kabisa.

Je, kiafya niko sahihi?
 
Hapana kabisa haupo sahihi! Kitaalamu inashauriwa ukinywa konyagi usinywe chini ya 1500mls kwa siku.
 
Kama %alcohol ni 35, ina maana unakunywa 8 units za alcohol. Kwa afya hiyo chupa inatakiwa kunywewa na wanawake 4 (unit 2 au pungufu, kwa mwanamke mmoja), au wanaume wawili (unit 4 au pungufu, kwa mwanaume mmoja). Na usinywe zaidi ya mara nne kwa wiki.
 
Pombe kali zinataka unywaji wenye discipline kali sana, ila ukienda kichwa kichwa lazima utaumia tu...
 
Unaweza kufafanua kidogo hayo mahesabu hapo mkuu?
 
Mimi Jumamosi na Jumapili nakunywa value kubwa 4 na safari lager 18.
 
Jana watu 3 tumelamba konyagi mbili kubwa, kreti la laiti na kitimoto kilo na nusu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…