Kipi ni Rahisi, serikali kutoa mabilioni kuwapa polisi ili kugharamia kuzuia maandamano ya siku moja au serikali kuamuru polisi kuwatafuta waliopotea?

Mwamuzi wa Tanzania

JF-Expert Member
Joined
Apr 7, 2020
Posts
15,486
Reaction score
45,256
Service ya magari ya maji ya kuwasha, ununuzi wa vilipuzi, risasi, posho za maaskari na maafisa wa jeshi la polisi ambao wamepatakaa barabarani leo ni kubwa sana. Hata kama hujui hesabu lazima utajua tu sio chini ya bilioni 2.
Huku vijana wa CHADEMA wanaosadika kutekwa hawazidi 20. Polisi Kuna kitengo cha kuwakomboa waliotekwa, rafiki yangu mmoja yupo kwenye kitengo hicho alipata mafunzo hapahapa Dar es Salaam.

Kwahiyo vijana wa jeshi la police 100 tu wangeweza kutosha kuwatafuta na kuwakomboa waliotekwa wote.
Kama hawajatekwa pia ni kazi ya polisi kuwatafuta na kusema wako wapi. Kama wamejiteka washikwe wapelekwe Mahakamani kwa mujibu wa Sheria.

Hii ya kutumia mabilioni kuzuia maandamano ya mtu ambaye hajashika hata fimbo haiingii akilini
 
Polisi wameonyesha kuwa Wanaresources za kuweza kuwapata wale wote waliotekwa lakini sijui kwa nini mambo yanaenda ndivyo sivyo.
 
athari za kutangaza kufanya maandamano kwa mihemko, kuchochewa na kuhamasishwa na kilevi 🐒
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…