Kipi wanacho makocha wa nchi za jirani ambacho makocha wenu hawana?

Kipi wanacho makocha wa nchi za jirani ambacho makocha wenu hawana?

bryan2

JF-Expert Member
Joined
Jun 8, 2016
Posts
3,323
Reaction score
4,679
Pale Stand United kuna Mrundi,Mbeya city kuna Mrundi pia,Simba nao kwa sasa kuna Mrundi,Yanga kuna Mzambia Lwandamina sijawataja Mromania wa Azam wala Hans Vans Plujim nimewataja makocha wa Nchi za Kiafrika tu waliomo nchini kwani nchi nyingi za Kiafrika tunafanana karibia kila kitu.

Makocha hawa sijui wamewazidi nini makocha wazalendo wa ndani ukiangalia kwa jicho la ndani zaidi ni makocha wachache sana kutoka kwetu wanaenda kufundisha timu za nje hasa za Kiafrika na tena wanakua makocha wasaidizi kuna Kocha Kama Kitambi alikua Kenya,Mkwasa naye alitoka kidogo ila sijasikia mwingine tena hata wakienda tu nchi za kawaida kama vile Rwanda,Burundi,South Sudan ambao atleast tupo nao level moja kisoka.

Najiuliza ni uwoga wa kujaribu kutoka na kutafuta Fursa sehemu nyingine au leseni zao haziruhusu nikimaanisha hawajafikia viwango vinavyotakiwa kufundisha mpira?
 
Tatizo tunaamini Tanzania hawawezi.Hata mchezaji akitoka nje atapewa muda mrefu na kusifiwa lakini jiulize kama Mavugo angekuwa Mtanzania leo angekuwa bado simba?
 
Tatizo ni kuwa they are not serious kwa ambacho wanakifanya wanaamini katika kipaji kuliko profesional, Niliwahi msikia kocha wa Mbao fc alisema alisoma miaka mitatu German kabla ya kuwa kocha kamili! sisi wabongo ujanja ujanja mwingi, hata kama wanavipaji hawana muda wa kusoma ili wawe na magamba yatayowapa mazingira mazuri kupata kazi nje ya nchi
 
Back
Top Bottom