BARD AI
JF-Expert Member
- Jul 24, 2018
- 3,591
- 8,826
Klabu hiyo imemfuta kazi Scott Parker aliyekuwa meneja wake ikiwa ni siku chache baada ya kufungwa magoli 9 - 0 dhidi ya Liverpool. Parker anakuwa kocha wa kwanza ndani ya Ligi ya England kufungashiwa virago tangu msimu ulipoanza.
Taarifa iliyothibitishwa na Mmiliki wa klabu hiyo, Maxim Demin imesema "Ningependa kuweka kwenye rekodi shukrani zangu kwa Scott na timu yake kwa juhudi zao wakati wa kukaa nasi. Kupanda kwetu kurejea Ligi Kuu msimu uliopita chini ya uongozi wake kutakumbukwa daima kuwa moja ya misimu yenye mafanikio zaidi katika historia yetu.
“Hata hivyo, ili tuendelee kusonga mbele kama timu na Klabu kwa ujumla, ni lazima tuwe sawa katika mkakati wetu wa kuendesha klabu kwa uendelevu. Ni lazima pia tuoneshe imani na heshima kwa wenzetu. Hiyo ndiyo njia ambayo imeiletea klabu hii mafanikio makubwa katika historia ya hivi karibuni, na ambayo hatutakengeuka kutoka sasa. Msako wetu wa kumtafuta kocha mkuu utaanza mara moja.”