john achila mukumwa
Senior Member
- Jan 4, 2024
- 142
- 281
Kipigo cha Wazaliwa wa Kwanza Kilichotokea Misri
Je umewahi kutafakari kwa nini mapigo yote 9 aliyopigwa Farao bado moyo wake ulikuwa mgumu? Na kwa nini lile pigo la 10 la kufa wazaliwa wa kwanza ndipo akawaruhusu wana wa Israeli?
Maana yake ni kuwa Farao aliendelea kuwa na moyo mgumu mpaka alipoingia kwenye ile bahari ya Shamu, na hapo ndiyo ikawa mwisho wake.
Ni kitu gani kilitokea mpaka Farao akawaachia wana wa Israeli?
Hiki si kingine bali ni ule msiba alioupata. Na huku bado moyo wake ukiendelea kuwa mgumu, alivunja sheria ya moyo wake na kuwafukuza wana wa Israeli. Lakini moyo wake bado uliendelea kuwa mgumu tu.
Kwanza tuangalie mapigo 9 kwa Misri yalikuwa ni yapi. Mapigo hayo yalihusu: 1. Damu, 2. Vyura, 3. Viroboto, 4. Nzi, 5. Vifo vya Mifugo, 6. Majipu, 7. Mvua ya Mawe, 8. Nzige, 9. Giza.
Tutazame maandiko katika kitabu cha Kutoka 11:1:
“BWANA akamwambia Musa, Liko pigo moja bado, nitakaloleta juu ya Farao na juu ya Misri; baadaye atawapa ninyi ruhusa mtoke huku; naye hapo atakapowapa ruhusa, atawafukuza mtoke huku kabisa kabisa”.
Siri gani iliyokuwepo ndani ya wazaliwa wa kwanza wa Misri hata kumfanya Farao awafukuze wana wa Israeli?
Kwani ni wazi kuwa hata Farao angepigwa kwa mapigo gani ya asili, asingewaachia wana wa Israeli.
Kitu gani kilikuwepo kwa wazaliwa wa kwanza wa Kimisri?
Kilichokuwa ndani ya wazaliwa wa kwanza wa Misri, ikiwemo mwana wa Farao, si kingine zaidi ya “miungu ya kimisri”.
Hivyo, kifo cha wazaliwa wa kwanza ilikuwa ni hukumu kubwa kwa miungu yao. Aidha, waliamini kuwa miungu yao ilikuwa ina nguvu nyingi.
Ndiyo maana MUNGU aliposhuka kuwaharibu wazaliwa wa kwanza, pia alisema ataiharibu na miungu yao. Kiuhalisia, miungu yao ilikuwa inaishi ndani ya hao wazaliwa wa kwanza.
Kutoka 12:12 “Maana nitapita kati ya nchi ya Misri usiku huo, nami nitawapiga wazaliwa wa kwanza wote katika nchi ya Misri, wa mwanadamu na wa mnyama; nami nitafanya hukumu juu ya miungu yote ya Misri; Mimi ndimi BWANA".
Zamani katika nchi ya Misri na hata katika mataifa mengine ya dunia, wazaliwa wa kwanza wa kiume waliaminika kama miungu ya familia na ya nchi. Na wanyama wa kwanza kuzaliwa, ndio waliotumika kwa kafara za miungu yao.
Hivyo watoto wote wa kwanza wa kiume walikuwa wanabeba ukuhani wa miungu, na roho zote za miungu zilikuwa zinakaa ndani yao.
KWA HIYO, KILICHOMWUMIZA ZAIDI FARAO SI MSIBA WA MTOTO, BALI NI KUHUKUMIWA KWA MIUNGU YAO ILIYOKUWEPO NDANI YA WALE WATOTO.
Farao alichanganyikiwa, hakuelewa ni nini kimetokea katika eneo lake la imani.
Na hata Wamisri wote walichanganyikiwa vivyo hivyo, hakuna ambaye hakulia. Wote walilia na kuhofu na kutoelewa ni nini cha kufanya. Waliyeyuka mpaka kufikia hatua ya wana wa Israeli kuwateka nyara.
Kutoka 12:33 “Wamisri nao wakawahimiza watu, kuwatoa katika nchi kwa haraka, maana walisema, Tumekwisha kufa sote.
34 Watu wakauchukua unga wa mikate yao kabla haijatiwa chachu, na vyombo vyao vya kukandia wakavitia ndani ya nguo zao mabegani.
35 Wana wa Israeli wakafanya kama neno lile la Musa; wakataka kwa Wamisri vyombo vya fedha na vyombo vya dhahabu, na mavazi.
36 BWANA akawajalia kupendelewa na Wamisri hata wakawapa kila walichokitaka. Nao wakawateka Wamisri nyara”.
NI UJUMBE GANI TUNAPATA HAPO? AU NI KITU GANI KILICHOKUWA KIMEWAFUNGA WANA WA ISRAELI?
Si utajiri wala hazina zilizoko Misri, kwa maana Bwana aliuharibu utajiri wake wote kwa zile mvua za mawe na nzige. Vile vile, si uzuri wa Misri, kwa sababu Bwana aliharibu uzuri wake kwa zile mvua za mawe, lakini bado wana wa Israeli walikuwa kifungoni.
Wala si ushujaa wa Wamisri, kwa sababu Bwana aliwapiga kwa chawa, na majipu na aliwanyima maji ya kunywa kwa siku saba. Hivyo, walikuwa dhaifu. Lakini bado wana wa Israeli walikuwa kifungoni.
Ni nini kilichokuwa kimewashikilia wana wa Israeli? Jibu ni miungu ya kimisri iliyokuwa inaabudiwa ndani ya watu. Hivyo, ilipopigwa pamoja na makuhani wake, ambao ndio wazaliwa wa kwanza, vifungo vikalegea, wana wa Israeli wakaachiwa.
Laiti Bwana Mungu angelileta hilo pigo mwanzoni kabla ya yote, Farao angewaachia Israeli kitambo sana, pamoja na moyo wake kuwa mgumu. Lakini Mungu aliliruhusu liwe mwisho wa kusudi lake maalum.
Na ukiendelea kusoma mbele utaona Bwana anawapa amri wana wa Israeli wawatakase wazaliwa wa kwanza, na kwamba kila mzaliwa wa kwanza atakuwa ni wa Bwana. Maana yake ni kuwa mzaliwa wa kwanza atakuwa kuhani wa Bwana kwa lazima, kwa sababu kulikuwa na kitu katika wazaliwa wa kwanza. Maana yake kila mzaliwa wa kwanza wa wana wa Israeli alipaswa kutolewa kwa Bwana, kama Hana alivyomtoa Samweli kwa Bwana. Kwa wakati huo, hiyo ilikuwa ni amri.
Hivyo, wazaliwa wa kwanza wa wana wa Israeli wanaozaliwa ilikuwa ni sharti wakombolewe kwa sadaka, ili watokane na kiapo hicho cha Bwana cha kuwa makuhani.
Na maana ya kukombolewa si kutolewa katika vifungo vya laana, kama baadhi ya mafundisho ya siku hizi za mwisho yanavyofundisha. Bali ukombozi ulikiwa ni ile hali ya mtoto kutolewa katika nafasi ya kikuhani ambayo angepaswa kuitumikia maisha yake yote.
Hivyo anapokombolewa anakuwa huru kama watu wengine wasio na utumishi wa kikuhani. Kwa ufupi anafunguliwa kutoka katika vifungo vya ukuhani. Na mtoto wa kwanza asipokombolewa, anabaki katika kifungo cha dhambi ya nafasi ya kikuhani.
Hata hivyo, sheria hiyo ilikuja kubadilika, na ukuhani wa wazaliwa wa kwanza likapewa kabila la Lawi, na siyo Waisraeli wote.
Maandiko katika kitabu cha Hesabu 3 kinasema:
12 “Mimi, tazama, nimewatwaa Walawi na kuwatoa kati ya wana wa Israeli badala ya wazaliwa wa kwanza wote wafunguao tumbo katika wana wa Israeli; na hao Walawi watakuwa wangu;
13 kwa kuwa hao wazaliwa wa kwanza wote ni wangu; katika siku ile niliyowapiga wazaliwa wa kwanza wote katika nchi ya Misri, nikajiwekea wakfu wazaliwa wa kwanza wote wa Israeli, wa wanadamu na wa wanyama; watakuwa wangu; mimi ndimi BWANA”.
Swali ni je, hata sasa katika agano jipya kuna sheria hizo za kukomboa mzaliwa wa kwanza?
Jibu ni hapana. Kwa sababu katika agano jipya hakuna sheria za kumkomboa mzaliwa wa kwanza au wa mwisho, kwa sababu wote waliomwamini Bwana YESU na kutakaswa kwa damu yake, wanafanyika kuwa makuhani wa Bwana.
Ufunuo wa Yohana 1:6 unasema: “na kutufanya kuwa ufalme, na makuhani kwa Mungu, naye ni Baba yake; utukufu na ukuu una Yeye hata milele na milele. Amina”.
Hivyo, wote tunayo huduma ya kikuhani mbele za Mungu, na ukishakuwa tu kuhani tayari ni mzaliwa wa kwanza bila kujali umri. Hivyo, kanisa la Kristo ni wazaliwa wa kwanza.
Waebrania 12:23 inasema “mkutano mkuu na kanisa la wazaliwa wa kwanza walioandikwa mbinguni, na Mungu mwamuzi wa watu wote, na roho za watu wenye haki waliokamilika”.
Kwa hiyo, hakuna sadaka yoyote ya ukombozi kwa wazaliwa wa kwanza kwa jinsi ya mwili.
Mafundisho na maombi ya kukombolewa kwa wazaliwa wa kwanza si ya kiMungu, bali ni ya ibilisi.
Ndiyo, tunaweza kuwaombea wazaliwa wetu wa kwanza na kuwaweka wakfu kwa Bwana, dhidi ya roho zinazofuatilia, lakini si kuwakomboa. Uwakomboe na nini? Je uwakomboe uwatoe katika ukuhani? Maana ndilo lengo la ukombozi. Hilo kibiblia lilikuwepo juu ya wana wa Israeli juu ya wazaliwa wa kwanza.
Zaidi sana, watoto wetu wa kwanza wanapaswa wawe wazaliwa wa kwanza kiroho kwa kumwamini YESU na kutakaswa ndipo wanapofanyika makuhani kama wengine wote waliomwamini YESU.
Kwa hiyo, fahamu kuwa kilichowafuga wana wa Israeli ni miungu ya Misri, iliyokuwa inaabimudiwa ndani ya kila kiumbe kilichokuwa cha kwanza.
KWA UJUMLA
1. Wana wa Israeli waliishi Misri kwa miaka 430. Kati ya hiyo, miaka 30 waliishi kwa amani na furaha, lakini miaka 400 iliyofuata, waliishi wakiwa kama watumwa. Kutokana na hali hiyo, Mungu aliamua kuwaokoa na kuwaondoa Misri.
2. Hata hivyo, Farao, ambaye ndiye alikuwa mkuu wa nchi ya Misri, aligoma kuwaruhusu Waisraeli kuondoka. Ndipo Mungu alipoamua kuachia mapigo kwa Misri, kwa lengo la kushinikiza Waisraeli kuachiwa.
3. Kulikuwa na mapigo 9, ambayo Farao alipata, lakini bado hakutaka kuwaachia Waisraeli. Pigo la 10 lilipopita, ndipo Farao alalazimika kuwaachia Waisraeli warudi kwao, katika nchi ya ahadi.
4. Ni nini kilitokea katika pigo la 10
Kilichotokea katika pigo la kumi ni ule msiba alioupata, wa kuuawa kwa wazaliwa wote wa kwanza wa binadamu na Wanyama, katika nchi nzima ya Misri.
Laiti Bwana Mungu angeliachia hilo pigo mwanzoni kabla ya yote, Farao angewaachia Israeli kitambo sana, pamoja na moyo wake kuwa mgumu. Lakini Mungu aliliruhusu liwe mwisho wa kusudi lake maalum.
5. Ni nini kilikuwa kimewashikilia Wana wa Israeli
Kilichokuwa kimewashikilia wana wa Israeli ni miungu ya Kimisri iliyokuwa inaabudiwa ndani ya watu. Hiyo ilipopigwa pamoja na makuhani wake, ambao ndio wazaliwa wa kwanza, vifungo vikalegea, wana wa Israeli wakaachiwa.