Kipimo cha maendeleo ni kuwa na gari

Hizo ndio akili za mafukara, subiria sasa hiko kipato kikue ufe

Kweli hakuna siku itafikia kipato kukutosha ,nadhani amesahau theory za fedha ,kwamba kadri kipato kinavyokuwa na matumizi yanaongezeka.
 

Kwa wenye familia gari ni muhimu sana hata kama hauna hela sana,kuna kushikwa na ugonjwa usiku wa maanani(manane) utaanza kumpigia uber? Mgonjwa atapanda bajaji? Kuna gari zipo hadi za mil 4 ,huyo huyo anayesema gari anasa lakini anakunywa pombe na kuonga mademu ukipiga mahesabu yaani kwa mwaka anaweza kutumia zaidi ya mil 10.
 

Ukiona mtu kanunua gari basi uwezo wa kujenga nyumba ni kama kumsukuma mlevi.

Gari unatoa hela zote moja kwa moja kama 15m unatoa hapo hapo ,hakuna oprtion ya kuanza kunua chassis au matairi au milango kisha ndio uunganishe , ila nyumba unaanza kununua kiwanja kwanza kisha unatulia ,unachimba msingi na kujenga foundation unatulia,unapandisha boma unatulia ,unaezeka na kuweka grill unatulia.
 
Huku kwetu ukinunua Gari unarogwa, siyo kwamba watu hawapendi kumiliki vitu vya aina hiyo ila tunahofia kuuwawa na watu wabaya wenye husda

Bora uwe normal tuu na siyo kufuata mkumbo
 
Pambana, mange kimambi na lemutuz hawana nyumba ila wana magari tu, na wanaongoza kwa kuwa na furaha nadhani kuliko hata kiumbe chochote hapa duniani.

Le mutuz ana nyumba mbili japo hazijaisha moja ipo Mbweni na nyingine kinyerezi hes humble you know hahaa ,mange hana kitu.
 
Mkuu gari inaogopwa kuliko nyumba, hamna uchawi pale, ni mambo ya hela tu, nyumba hata ya matope unajenga kwa laki tano tu fukayosi huko

Ukitaka kujua gari inatisha ,wewe jenga mansion la maana halafu uwe hauna gari,masela watasema jamaa amewekwa alinde nyumba ya broo wake yupo marekani.😀😀😀😀😀😀😀.
 
Baelezee hayo mafukara
 
Huku kwetu ukinunua Gari unarogwa, siyo kwamba watu hawapendi kumiliki vitu vya aina hiyo ila tunahofia kuuwawa na watu wabaya wenye husda

Bora uwe normal tuu na siyo kufuata mkumbo
Hawakufanyi chochote we vuta mkwaju tu hata kama ni tu porte namba A urudishe heshima mtaani
 
Kuna pisi kali juzi imeshindwa kwenda kazini na BMW yake, ikaniambia ukweli nimeamua kutulia home sina hata buku kumi ya mafuta,mnyamwezi nikaiambia ungesema mapema mamayo zako.
Kawaida tu kumbuka siku nyingine inakuwaga full tank hiyo mzee, hiyo ilikuwa hali ya kupita tu
 
Gari ni asset sasa kwanini isiwe sehemu ya mavuno ya mafanikio na kupiga hatua
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…