Kipimo cha maendeleo ni kuwa na gari

Kipimo cha maendeleo ni kuwa na gari

Hizo ndio akili za mafukara, subiria sasa hiko kipato kikue ufe

Kweli hakuna siku itafikia kipato kukutosha ,nadhani amesahau theory za fedha ,kwamba kadri kipato kinavyokuwa na matumizi yanaongezeka.
 
Kabla ya kununua Gari kaa chini na piga hesabu unataka kufikia wapi kwenye maisha yako? una malengo gani? na je gari itakusaidia kufikia malengo yako? kama unanunua gari kwa ajili kukwepa kupanda daladala, kujionyesha na wewe unazo, hapo umekosea na hio gari itakufanya maskini, number hazidanganyi kaa chini, piga hesabu ya kipato, gawanya kwa matumizi yako, ya maendeleo,ya kununua gari, na kulihudumia gari, ukipata jibu ndio ufanya uamuzi

Kwa wenye familia gari ni muhimu sana hata kama hauna hela sana,kuna kushikwa na ugonjwa usiku wa maanani(manane) utaanza kumpigia uber? Mgonjwa atapanda bajaji? Kuna gari zipo hadi za mil 4 ,huyo huyo anayesema gari anasa lakini anakunywa pombe na kuonga mademu ukipiga mahesabu yaani kwa mwaka anaweza kutumia zaidi ya mil 10.
 
Gari itakupa heshima binafsi mjini (japokuwa inaweza kukupa umaskini pia ukijichanganya). Nyumba ni urithi wa kudumu kimaisha katika familia. Kuna namna fulani mtu anakuwa na utulivu wa ndani akiwa anaishi kwake. Na kuna namna fulani hivi ya kujisikia ufahari na kujiamini ukiwa unamiliki gari.

Ukiona mtu kanunua gari basi uwezo wa kujenga nyumba ni kama kumsukuma mlevi.

Gari unatoa hela zote moja kwa moja kama 15m unatoa hapo hapo ,hakuna oprtion ya kuanza kunua chassis au matairi au milango kisha ndio uunganishe , ila nyumba unaanza kununua kiwanja kwanza kisha unatulia ,unachimba msingi na kujenga foundation unatulia,unapandisha boma unatulia ,unaezeka na kuweka grill unatulia.
 
Huku kwetu ukinunua Gari unarogwa, siyo kwamba watu hawapendi kumiliki vitu vya aina hiyo ila tunahofia kuuwawa na watu wabaya wenye husda

Bora uwe normal tuu na siyo kufuata mkumbo
 
Pambana, mange kimambi na lemutuz hawana nyumba ila wana magari tu, na wanaongoza kwa kuwa na furaha nadhani kuliko hata kiumbe chochote hapa duniani.

Le mutuz ana nyumba mbili japo hazijaisha moja ipo Mbweni na nyingine kinyerezi hes humble you know hahaa ,mange hana kitu.
 
Mkuu gari inaogopwa kuliko nyumba, hamna uchawi pale, ni mambo ya hela tu, nyumba hata ya matope unajenga kwa laki tano tu fukayosi huko

Ukitaka kujua gari inatisha ,wewe jenga mansion la maana halafu uwe hauna gari,masela watasema jamaa amewekwa alinde nyumba ya broo wake yupo marekani.😀😀😀😀😀😀😀.
 
Ukiona mtu kanunua gari basi uwezo wa kujenga nyumba ni kama kumsukuma mlevi.

Gari unatoa hela zote moja kwa moja kama 15m unatoa hapo hapo ,hakuna oprtion ya kuanza kunua chassis au matairi au milango kisha ndio uunganishe , ila nyumba unaanza kununua kiwanja kwanza kisha unatulia ,unachimba msingi na kujenga foundation unatulia,unapandisha boma unatulia ,unaezeka na kuweka grill unatulia.
Baelezee hayo mafukara
 
Huku kwetu ukinunua Gari unarogwa, siyo kwamba watu hawapendi kumiliki vitu vya aina hiyo ila tunahofia kuuwawa na watu wabaya wenye husda

Bora uwe normal tuu na siyo kufuata mkumbo
Hawakufanyi chochote we vuta mkwaju tu hata kama ni tu porte namba A urudishe heshima mtaani
 
Kuna pisi kali juzi imeshindwa kwenda kazini na BMW yake, ikaniambia ukweli nimeamua kutulia home sina hata buku kumi ya mafuta,mnyamwezi nikaiambia ungesema mapema mamayo zako.
Kawaida tu kumbuka siku nyingine inakuwaga full tank hiyo mzee, hiyo ilikuwa hali ya kupita tu
 
Asikudanganye mtu wala kukutia moyo, kama wewe huna gari hata kama ni mkweche unahesabika ni fukara tu hata kama una nyumba 50, tafuta gari upate amani ya moyo na heshima kwa wakwe hata kama huna hela.

Muhimu kujilinda, korona ipo na inaua fuateni miongozo ya wataalam wa afya jamani.

Kzba.
Gari ni asset sasa kwanini isiwe sehemu ya mavuno ya mafanikio na kupiga hatua
 
Back
Top Bottom