Kipimo cha tezi dume

alex50

JF-Expert Member
Joined
Jan 28, 2008
Posts
217
Reaction score
114
Kipimo cha tezi dume ni cha kumdhalilisha anaepimwa kwa maoni yangu. Maana nmeambiwa ni lazima dokta aingize kidole mkunduni.
Hivi inawezekana nikajipima mwenyewe nikipewa maelekezo? Ma Dr naomba kujuzwa.
 
Uongo huo usituletee Story Za Viroba hapa Kama Unashindwa Hata Kugoogle au KuYouTube ukajifunza mwenyewe..
Haya inama Basi ujitie Hicho Kidole Cha Lusindo ujikaguwe hiyo Tenzi Dume Yako...
 
That's the most cost common and the most used method, kupima tezi dume lazima ufanyiwe DRE "digital rectal examination" na wala sio udhalilishaji ni zoezi la kawaida sana, pia sio kupima tezi dume tu ni moja ya part ya GIT system examination (uchunguzi wa mfumo wa chakula) ambapo DRE hutumika kuedetermine kama kuna tatizo lolote katika rectum (puru) ,kwa hiyo usiogope mkuu ni njia ya kawaida kabisa sawa na kupima mapigo ya moyo tu
 
Ugonjwa huu dalili zake ni nini mnaojua Mana naona ulimpata JK na sasa umemuondoa Sitta
 
Uongo huo usituletee Story Za Viroba hapa Kama Unashindwa Hata Kugoogle au KuYouTube ukajifunza mwenyewe..
Haya inama Basi ujitie Hicho Kidole Cha Lusindo ujikaguwe hiyo Tenzi Dume Yako...
Kipimo ndio hicho aisee msikatae ila nafikiri kuna zaidi ya hicho but could the intial tests
 
Mimi sio daktari lakini hiki ndicho ninachojua kuhusu saratani ya tezi dume na vipimo vyake:

  • Tezi dume ikianza kuvimba utajua tu kwa sababu utaanza kuwa na shida ya kukojoa. Lakini hali hii saa nyingine inajitokeza wakati saratani imejieneza mwilini.
  • Njia ya kutumia kidole kwenye rectum ndio njia rahisi kwa daktari kuona kama tezi yako imevimba au la (hata kabla ya kushindwa kukojoa).
  • Njia nyingine ya kuona kama saratani imeanza katika tezi yako ni kupima antigen (protein) inayotolewa na hii tezi hasa kama ina saratani. Kipimo hiki kinaitwa PSA (Prostate-Specific Antigen) test. Kufanya kipimo hiki kinahitaji maabara maalum na kuna taarifa kuwa kipimo hiki saa nyingine sio cha kuaminika sana.
  • Unaweza pia kufanyiwa uchunguzi wa saratani ya colon (colonoscopy). Wakati wakifanya hii colonoscopy wanaweza pia kuona kama tezi yako imevimba au la. Kipimo hiki kinahitaji vifaa maalum na ni ghali.
Wanaume wote wenye umri wa zaidi ya miaka 50 nawashauri wavumilie tu kuchekiwa kwa kidole, labda mara moja kila baada ya miaka 5. Madaktari wenye taaluma yao wanaweza kunisahihisha.

Ni muhimu tuelezane/tushauriane vema kwa sababu huu ni ungonjwa unaotibika kabisa kama ukigunduliwa mapema.
 
Hicho kipimo ndio kinasababisha mauti kwa wanaume wengi sana, kwa nini mtu uogope kupimwa hivyo na wanaume wenzako ma dokta wakati unamuacha mkeo anaenda kuimwa njia wakati wa kujifungua hata na madokta wa kiume? ifike mahali matibabu yakubalike kuepusha vifo visivyo vya lazima.
 


Mkuu Mwanamke Kupimwa Njia Ni Sahihi Kwani Hata Akafikia Kubeba Ujauzito Ni Kuwa Pale Pahali Pameshatiwa Dudu Sana tu! Na Ndiyo Nature Yake Pale Kutiwa.... Kwahiyo kutiwa Hakuanza Siku Ya Kupimwa Njia..

Lakini Mwanamme Ukamuinamishie Mwanamme Mwenzako Akutie Kidole Kilainilaini Hivyo Wakati Sio Nature Yake Kuingizwa Kitu..! Dah Hapo Mkuu Mimi Bora Nife Na Maradhi Nitaridhika Kuliko Kipimo Hicho...
 
Kipimo cha tezi dume ni cha kumdhalilisha anaepimwa kwa maoni yangu. Maana nmeambiwa ni lazima dokta aingize kidole mkunduni.
Hivi inawezekana nikajipima mwenyewe nikipewa maelekezo? Ma Dr naomba kujuzwa.
Ntafute mimi napima kwa macho tuu,njoo usiogope
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…