elder mamba
New Member
- Apr 27, 2024
- 1
- 0
Katika hali ya kushangaza na kusikitisha kumekuwa na mahususiono mengi ambayo yamejawa na kutokuaminiana ndani yake, maana yake nini? Tangu kuumbwa kwa ulimwengu huu suala la kutokuamiana hasa kwa viumbe hai limekuwa sugu sana na hasa kwa kiumbe aitwaye mwanadamu.
Mwanadamu huyu aliyeumbwa kwa uzuri kabisa na kupewa kila aina ya mvuto na akili timamu, mvuto ambao umeambatana na kiasi kikubwa sana cha hisia nzurii za mapenzi kwa binadamu mwenzake hasa jinsia tofauti.
Hali inayonipelekea mimi mwandishi kuamini ya kwamba huyu kiumbe mwanadamu kwa jinsia yake tofauti lazima atatafuta kuwa na mahusiano ya kimapenzi na binadamu mwenzake wa jinsia tofauti iwe kwenye ndoa au hapana mtaalamu mmoja alisema (universal pleasure).
Mara nyingi tunaposhiriki katika tendo hili wengine wakijinasibu kwa kuita tendo takatifu kwa wanandoa na wengine kama mwandishi nikiita zinaaa. Tendo hili limekuwa na Baraka nyingi sana na sehemu kidogo ya laana.
Miongoni mwa baraka nyingi hasa tunaposhiriki katika tendo hili ni kwa ajili kuijaza dunia(kupata watoto) na wakati mwingine vijana wakisema nikupeana joto hali ambayo mwisho wa siku wote wawili binadamu wa kike na wakiume wanakuwa na akili timamu.
Ambatana na mimi hasa kwenye baadhi ya laana chanche ambao mwndishi wako leo natamani uzijue maana na hizi nazo zimekuwa nyingi sana hasa kiumbe mwenye jinsia ya ke/me kuamua kujitoa uhai wake pale ambapo miongoni mwa ahadi waliozoaidiana wakati wa mahusiano kutokutimizwa na wengine kusabisha kuwatoa uhai binadamu wenzao kwa sababu tu amelala na mke/ mme wake jamiii ikiita ni wivu wa kimapenzi. Hali hii imepelekea kuwa na matukio mengi ya ukatiri wa kijinsia kwa watoto, wanawake na wanaume pia.
Kubwa kabisa ambalo nimeona leo niwasogeee wanajamii forum wenzangu mbali na utamu uliojaa katika mapenzi ni mvulugano wa wanandoa na wapenzi pale mwenza wa kike anapokuwa mjamzito au amekwisha kujifungua mtoto/watoto. Mvulugano huu unaletwa na kitu kikubwa kiitwacho mashaka(doubt) ambacho huenda kimesababishwa na kukosekana kwa imani miongoni mwa wapendanao hawa au jamii imeeamua kuwafalakanisha wapendano hawa upande mmoja ukidai mtoto sio wake au wa kwao.
Nashawishika kuamini ya kwamba wewe kama baba au mtarajiwa kuna siku moja ambayo haijawahi kupewa jina ulikumbwa na wimbi kubwa la mashaka kuhusiana na uhalali wa mimba au watoto ulionao na kizuri zaidi katika dunia hii mama ndiye kiumbe pekee mwenye uhalali wa kuitwa mama wengine wakaenda mbali zaidi wakisema (there is no biological fathers). Hali hii imepelekea wimbi kubwa la huitaji wa vipimo vya vinasa saba jambo ambalo ni jema kwa maana ya uhalali wa mtoto na pia amani ya moyo pale mnapokuwa mnapambana usiku na mchana kwa ajili ya kutafuta lizikizi ya familia yake.
Changamoto zitokanazo na wimbi hili kubwa kama ambavyo nimegusia hapo juu mimi mwandishi wenu ni usitawhi mbovu wa familia, watoto hasa kuanzia kiafya,kielemu na hata imepelekea ndoa nyingi kuvunjika wengine wakisema hawawezi kuhudumia damu isiyo yao wengine pia wakapata nafasi ya kuwasilisha mabadiliko ya umilikishwaji pindi mtoto anapokuwa mkubwa baada ya haliya maisha kuyumba kwa mwenza mmojawapo. Uwepo wa huduma hii muhimu itapunguza kelo kwa wananchi hasa wale ambao wamekuwa kwenye wimbi kubwa la mashaka pia itaongeza uaminifu kwa wanandoa na kupunguza matukio mengi ya ukatiri wa kijinsia jambo ambalo jamii inapaswa kubadilika na kulipokea jampo wengi huamini ya kwamba itaongeza mvulugano wa familia. Tunaitaji kufanya tafiti juu ya ukubali wa upatikanaji wa vipimo hivi kwa kushirikiana na mamlaka.
Zipo mamlaka kamili zenye kusimamia suala la upatikanaji wa vipimo vya vinasaba kwa wananchi wenzetu ambao wamekumbwa katika kazia hii, ambapo mlolongo wake huusisha vyombo vya sheria kupitia ofisi za ustawi wa jamiii. Mamlaka hizi mbili zishirikiane katika kuendelee kutoa elimu kwa jamiii yetu ya kitanzania lengo ikiwa ni ustawi bora wa watoto katika taifa letu sambamba na kupungua vitendo vya ukatili kwa watoto na wanandoa na namna bora ya kupata huduma hii. Sambamba na mabadiliko chanya ya kisera na mifumo ya upatikanaji wa huduma hii pasipo kuwa na ukiritimba kwa wanandoa hawa hasa pale taratibu zinpofuatwa lengo ikiwa kupunguza yasiyotarajiwa( sababu wivu wa mapenzi).
Suala la uaminifu kwa wanandoa au wapenzi ni jambo la msingi sana ambalo linaweza kuwa na kiwango kikubwa sana katika kutokomeza athari zozote zile zitokanazo na kutokuamiana kwa wanandoa hawa. Hapa ndo kazi ilipo na ndio shina la tatizo kwa hiyo Serikali iwekeze hapa kwa kushirikiana na viongozi wa dini ili tupate jamii yenye kuaminiana. Ikishidikana katika hili basi huduma wezeshi ya kuondoa utata kwa kufanya vipimo vya vinasaba ipatikane kwa maana hakuna mtoto ambaye hana baba na mamlaka itusaidie kupitia mwenzi ili baba apatikane na awajibike katika malezi ya mtoto wake. Huenda changamoto kubwa ni kuwa na usiri wa muhusika maana huenda kuwa jirani, rafiki au ndugu.
Elimu ya upatikani wa huduma ya vipimo kwa wananchi iendeleee kutolewa ikiwa ni pamoja na kuanisha vipaumbelee vya msingi kwa kujali ustawi wa familia na watoto. Na kwa wale wazazi wanaokataa mimba itakua rahisi kwao pia kwa mamlaka kuchukua hatua za mkondo wa sheria pale ambapo imebainika yeye kuwa mhusika mkuu.
Mwisho jamii kurudi katika misingi ya kuamiana kila mmoja kwa nafasi yake lengo kubwa kupata familia ambayo haina mashaka ndani yake na wala watoto wasiopata changamoto zozote katika makuzi na malezi ili tupate jamii yenye ustawi bora.

Upvote
1