Kipindi Bora zaidi cha Television na Radio Tanzania...

Kipindi Bora zaidi cha Television na Radio Tanzania...

Mimi huko nyuma nilipenda mama na mwana na yule mbibi akitusomea hadithi ni nzuri sana - RADIO TANZANIA kwasasa
Ni tbc.
Tv ni ITV kipindi ni filamu saa nne hasubuhi ya watoto wetu inaitwa Wou Kung yule kima.
Hata Egoli na filamu za saa nne usiku nyingi nzuri sana kama acapulco bay jumong na Larevanger na nyingine nyingi.
 
Nikiwa mdogo nilikuwa napenda kusikiliza kipindi kinaitwa miwani ya maisha kilikuwa Radio one mama alikipenda sana!!...!kilikuwa jumapili mimi nilikuwa naandaa viatu vya shule kwa kuvipaka rangi/kiwi orijino ile na yeye alikuwa akipika au kufanya chochote. Radio nilikuwa naambiwa kuileta jikoni nami naketi mlangoni. Kilikuwa kipimdi cha kusisimua sana. san
 
Kiss kolabo ya zamani...kuna madam flan ivi alikua anakiendeshe pale kiss fm anasauti nzito ivi nilikua napenda sana enzi izo kwa sasa amna kitu

Afro jam ya enzi izo kiss fm

Kwasasa ni the cruzzy EARD

mimi ni mpenzi sana wa redio kuliko tv
 
Hapo upande wa radio #2 Kiss Fm early 2006/10 palikuwaga na kipindi fulani cha kucheza ngoma kali {old school} za nje na za ndani za miaka hiyo kuanzia saa 8 mchana hadi 10 jioni mtangazaji wake akiitwa kitu kama Kim,sijui jamaa yupo wapi kwa sasa ila hiki kipindi na huyu presenter nilikuwa namkubali sana.

Unaweza kujua huyu jamaa yupo redio gani kwa sasa mkuu?hawa RFA nao kama ni wamechoka tu maana hata Kiss Fm yenyewe sijui kama bado ipo.
 
Soso fresh ya clouds fm kila wkend,kuna michano ya freestyle hatari pale.
 
Hapo kwenye chombeza time, Ongezea na kile cha jumapili usiku ilijulikana kama kipindi cha RAFIKI chini ya ROSE CHITALA kulikuwa na Love story hizoo!! ROSE CHITALA yupo wapi?

Uongozi wa Radio One - Deo Liyunga mnaharibu sana kipindi cha rafiki cha kila Jumapili ,Sisi ni wafatiliaji sana tangu enzi za Rose Chitara,akaja Kaka Mohamed ila kwasasa yupo DJ niko track aiseee yaani tulizoea music laini na mikasa ya kimapenzi ila kwasasa kipindi cha rafiki yaani ni kama Hiphop hakina tofauti na DJ Show ,The Cruz au XXL.

Shida ni nini? Bora mumrudishe Amina Chengo au Abubakari sadiq kwenye hicho kipindi ,DJ niko traki hakiwezi kukirun hicho kipindi.
 
1.sitasahau ya Rfa kabla ya 2010
2.kuna kipindi nimesahau jina kilikuwa kinaanza saa 2-3 asubuhi kabla ya sitasahau pale Rfa mtangazaji akiwa rebecca mresi au Roy maganga
° Saa 2 hadi 3 Ushauri wako
° 3 hadi 3.5 Je wajua
° 3.5 hadi 4 je huu uungwana
° 4 hadi 5 sitasahau

Sijui kama walibadilisha ratiba maana mimi toka 2012 ilipoanza kutikisika sijasikiliza kwa umakini.
 
Back
Top Bottom