Kipindi cha Clouds 360 ina ujuaji uliopitiliza mpaka wasichokijua

Kipindi cha Clouds 360 ina ujuaji uliopitiliza mpaka wasichokijua

Hao jamaa wanaeleweka vizuri tu, kwanza ni wabunifu. Clouds wote ni wabunifu wa vipindi vyao ndio maana wanaigwa sana na wengine. Clouds media wameamua kujitofautisha na wengine hata usomaji wa taarifa ya habari uko tofauti na wengine.

Hicho kipindi cha 360 ni kipindi kimoja cha asubuhi chenye segment nyingi ndani yake ikiwemo uchambuzi habari magazetini. Huo uchambuzi wa habari magazetini tu ni tofauti na wengine wanaosoma vichwa vya habari kwa haraka na kupita bila kueleweka.

Huyo jamaa bonge kwenye hicho kipindi kusimaa kwake mwanzo mwisho bila kukaa ni ubunifu tosha japo wengine nao wameiga staili hiyo. Kwa ujumla clouds media wamekuwa role model kwa wengine kuiga ubunifu wa vipindi vyao japo tasnia ya habari ni sanaa ingawa haitambuliwi na BASATA kama ni sanaa.

kupe
 
Back
Top Bottom