Kipindi cha kampeni wanasiasa wanakuwa na masikio

Kipindi cha kampeni wanasiasa wanakuwa na masikio

Sky Eclat

JF-Expert Member
Joined
Oct 17, 2012
Posts
57,761
Reaction score
216,011
Kipindi cha kampeni kinakaribia. Katika kipindi hiki nchi inakuwa pepo ndogo. Shida zinasikilizwa na ahadi kutolewa.

Achana na zile shida kubwa kama ujenzi wa zahanati, maji, umeme barabara na shule. Hizi ni shida ambazo tumeziimbia ngojera tangu baada ya uhuru na tunaendele kuzikariri.

Ni zile shida binafsi kama ada ya mtoto. Hasa ukiwa na ushawishi katika kikundi fulani Mgombea hatakulipia ada tu atakwambia melete kijana mjini kesho saa mbili asubuhi. Atanunuliwa viatu vya shule na socks, sare ya shule na madaftari. Mtoto atashangaa kumbe huyu ni anko lakini miezi sita iliyopita hakuwa hata anaulizia hali ya baba tukionana!!

Hii ni miezi mgombea akijua wewe unaushawishi kwenye jamii fulani, atajitolea kuezeka bati kwenye nyumba ya shangazi yako mjane. Hawa wasamaria humaliza kazi yao ya usamaria kura zikisha hesabiwa.
 
Back
Top Bottom